RIO FERDINAND KUSAKA VIPAJI TANZANIA, MAKONDA AFUNGUA MILANGO YA ULAYA KWA VIJANA WA SOKA

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Richard Poul. May 22 Mwaka 2026 .

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda amesisitiza kuwa ziara ya mwana Soka Rio Frerdnand,italeta fursa kwa vijana wenye ndoto ya kukua kwenye mpira wa miguu kupata nafasi ya kukuza vipaji vyao.

Taarifa hiyo ameitoa leo, Mei 22, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ujio wa nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza,Reo Ferdinand.

Habari Picha 18522

Waziri Makonda amesema ndoto yake kubwa ni kuona wachezaji wakubwa wakichukua vijana na kuwapeleka Ulaya kuwaendeleza ambapo alianza na Drogba na kufuatiwa na Rio ambaye ana mtandao mkubwa wa watu wa karibu wenye utaalamu wa michezo na biashara,hivyo ni rahisi kuwapeleka vijana nje ya nchi kusakata kabumbu ya kulipwa.

“Ndoto yangu kubwa ilikuwa Reo aje nchini kusaka vipaji vya watoto na awachukue,leo hii atatuma timu yake ya wataalamu kwenda Qatar kuangalia vijana wetu wa chini ya umri wa miaka 17,ambao wanashiriki kombe la Dunia, watakaofanya vizuri atawachukua” amesema Waziri Makonda.

Naye Rio Ferdinand amesisitiza azma yake ya kuwainua watoto wa Kitanzania wenye vipaji vya soka kupitia taasisi yake iliyopo nchini Uingereza, ambayo inalenga kuwapa vijana fursa ya kukuza vipaji vyao kwa viwango vya kimataifa.

Habari Picha 18523

Aidha mwanasoka huyo ameshukuru mapokezi makubwa ayenye ukarimu yaliyofanywa na Watanzania wakiongozwa na Rais Dkt Samia Sululu Hassan pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Paul Makonda.

Weka headline yenye mvuto

Share This Article
Leave a Comment