SIKU YA PENTEKOSTE: KUSHUKA KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU YA MABADILIKO

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Geofrey Stephen Arusha .

Leo katika ibada iliyoongozwa na Alex Rafael katika Kanisa la KKKT Usharika wa Salei Mtaa Levolosi, Jijini Arusha Somo la siku lilikuwa kuhusu kushuka kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste.

Habari Picha 18433

Mafundisho yalieleza maana ya Pentekoste kuwa ni siku ya hamsini baada ya ufufuo wa Yesu Kristo. Neno “Pentekoste” limetokana na lugha ya Kigiriki likimaanisha “hamsini,” baada ya kutimia kwa majuma saba kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Walawi.

Habari Picha 18427

Katika mafundisho hayo, waumini walikumbushwa jinsi Yesu alivyowatayarisha wanafunzi wake kwa maombi, subira, na kutafakari Neno la Mungu hadi siku ile Roho Mtakatifu aliposhuka juu yao kwa nguvu kubwa.

Ilikuwa siku ya mabadiliko makubwa  siku ambayo hofu ilibadilika kuwa ujasiri, mashaka yakageuka kuwa imani, na maisha ya kawaida yakajazwa nguvu na uwepo wa Mungu.

Habari Picha 18429
Habari Picha 18428

Mahubiri yalisisitiza kuwa Pentekoste si tukio la kihistoria pekee, bali ni mwaliko kwa kila Mkristo kuishi maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu kila siku. Kuwa na Roho Mtakatifu kunamaanisha kuwa karibu na Mungu, kulitafakari Neno lake kwa bidii, kuishi katika upendo, amani, utakatifu, na kutembea katika njia zake.

Habari Picha 18430

Baada ya mafundisho hayo, mioyo ya wengi iliguswa sana. Kulikuwa na hali ya utulivu na tafakari ya kina, huku wengi wakijiuliza ndani ya mioyo yao: “Je, kweli Roho Mtakatifu ana nafasi katika maisha yangu?” Waumini walihamasishwa kuongeza bidii katika maombi, kusoma Neno la Mungu, na kumruhusu Roho Mtakatifu kuwa mwongozo wa maisha yao ya kila siku.

Habari Picha 18424

Pentekoste hutukumbusha kuwa Mungu bado anasema na watu wake, bado anawainua waliokata tamaa, na bado anawasha moto wa imani ndani ya mioyo ya wale wanaomtafuta kwa kweli. Kama wanafunzi wa Yesu walivyobadilishwa na nguvu ya Roho Mtakatifu, vivyo hivyo nasi tunaweza kubadilishwa na kuwa mashahidi wa upendo, imani, na nguvu za Mungu katika dunia ya leo.

Habari Picha 18432
Habari Picha 18425
Habari Picha 18434

Mwisho.

Share This Article
Leave a Comment