Na Richard Poul .
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kupata Kichwa Cha aliyekuwa Mwanafunzi wa chuo Cha usimamizi wa Fedha (IFM) James Temba ambaye hivi karibuni mwili wake ulikutwa ukilelea kwenye maji Mto Msimbazi.
Taarifa hiyo imetolewa l Mei,13,2026 Jijini Dar es salaam na Kamanda Kanda Maalumu ya Dar es salaam SACP Jumanne Muliro wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Aidha amesema kuwa baada ya upelelezi wa kina kufanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya upelelezi wa kisayansi,sehemu ya Kichwa hicho kimepatikana eneo la Kitunda Kibeberu Wilaya ya Ilala kikiwa kimefukiwa ardhini.
“Hadi sasa Watu watano wamekamatwa,akiwemo mganga wa kienyeji anayejulikana kwa jina la Saidi Ally(Side)Mzigua (31)” amesema SACP Muliro
Nakuongeza kuwa”Taratibu za kisheria zinakamilishwa ili watuhumiwa wafikishwe kwenye Mamlaka za kisheria.”
Aidha amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwashukuru Wananchi na Mamlaka zingine za uchunguzi wa kisayansi katika kufanikisha zoezi la upatikanaji wa Kichwa hicho.
“Jeshi la Polisi linawataka Wananchi kuacha kutoa taarifa za upotoshaji wakati uchunguzi wa matukio ya kiuhalifu ikiwemo mauaji unaendelea.”
Hata hivyo Jeshi hilo linaendelea kulaani watuhumiwa waliotekeleza mauaji hayo nakwamba litaendelea kufuatilia jarada la kesi hiyo ili watuhumiwa wapate adhabu wanayostahili.

