ANAANDIKA GODBLESS LEMA NAMNA YA KUCHANGIA CHADEMA

Geofrey Steven
2 Min Read

Katika mjadala unaoendelea kuhusu mchango wa wananchi katika shughuli za kisiasa, mwanasiasa na mwanaharakati Godbless Lema amesema kuwa nguvu ya mabadiliko nchini haiwezi kutegemea viongozi pekee, bali pia uwezo wa wananchi na wanachama wa vyama vya siasa kujitolea kifedha kwa ajili ya kuendesha shughuli za kisiasa na harakati za maendeleo.

 

Habari Picha 18222

Lema amesema vyama vya siasa, ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), vina uwezo mkubwa wa kujitegemea kifedha iwapo wanachama na wafuasi wake watakuwa na nidhamu ya kuchangia kwa ajili ya shughuli za chama na mapambano ya haki na demokrasia.
Ameeleza kuwa changamoto kubwa iliyopo si ukosefu wa fedha pekee, bali ni mtazamo wa jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia shughuli za pamoja. Kwa mujibu wake, wananchi wengi wana uwezo wa kutumia fedha nyingi katika sherehe na shughuli binafsi za kifahari, lakini hushindwa kutoa michango hata midogo kwa ajili ya kusaidia wagonjwa au kuimarisha harakati za kisiasa na kijamii.
Kwa mtazamo wake, hali hiyo inaonyesha kuwa tatizo kubwa lipo katika fikra na vipaumbele vya jamii kuliko hata changamoto za kikatiba au kisiasa.
Lema ametoa wito kwa Watanzania wenye nia ya kuona haki, maendeleo na demokrasia ya kweli nchini kuwa na moyo wa kujitolea kifedha ili kusaidia uendeshaji wa vyama vya siasa na harakati za mabadiliko.
Aidha, amesema kuwa ni jambo linaloumiza kuendelea kuomba michango kwa jamii ambayo inapaswa kuelewa kuwa kuendesha vyama vya siasa ni wajibu wa wanachama na wafuasi wake wenyewe

Share This Article
Leave a Comment