baraza la madiwani lataka mazao ya wakulima kulindwa dhidi ya wanyama waharibifu wakiwamo Tembo

Geofrey Steven
3 Min Read

Na Bahati Siha,

Baraza la Madiwani Halmshauri ya Siha mkoa wa Kilimanjaro,limeagiza Ofisi ya Mkurungenzi mtendaji wa Halmshauri hiyo,Helleni Mwambeta kuhakikisha inawawezesha vifaa maafisa wanyamapori ili kuwathibiti Wanyama wasiingie kwenye mashambani na kuharibu mazao akiwamo Tembo

Haya yapo kwenye taarifa yake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Dancan Urasa aliyoitwa Mei ,6,2026,kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2026,kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

 

Habari Picha 17983
Habari Picha 17976

Katika taarifa yake Mwenyekiti hiyu,ameagiza Mkurungenzi mtendaji wa Halmshauri,kuhakikisha anawezesha kitengo hicho cha Wanyamapori ili waweze kuwathibiti Wanya hao ambao kila mwaka wamekuwa wakiharibu mazao mbali mbali ya wakulima yakiwemo mahindi maharage na alizeti maeneo mbali mbali wilayani humo

“Ni kweli tumeagiza jambo hili lifanyike kwa haraka ,kwani zipo taarifa kwamba Tembo wameshaanza kuingia kwenye mashamba na kuanza kuharibu mzao hatuwezi kukaa kimiya tukiangalia chakula kikiharibiwa kwa sababu sisi ni wawakilishi”amesema Dancan

Dancan amesema kila mwaka wakulima wamekuwa wanafanya jitihada za kilimo ili kupata mazao ya kutosha ya biashara na chakula kwa lengo la kuendesha maisha yao lakini wamekuwa wakikatishwa tamaa na wanyama hao kwa kuingia shambani na kuharibu bila kujua gharama walizotumia

Amesema mwaka huu hawata kubali kuona mkulima anapata hadara , lazima Maafisa hao wa Wanyapori wasimame vizuri kuweka ulinzi wa kutosha ,mvua zimenyesha za kutosha ,wakulima wamelima kisasa ,wameweka mbolea kwa hiyo kuna chakula cha kutosha Mungu akipenda,

Haya mazao mengine nje ya chakula pia ni ya biashara ,hivyo yanachangia kuongeza mapato ya Halmshauri,hivyo ni muhimu kuweka nguvu katika jambo ili Wilaya iwe na maendeleo

Rehema Lukumai mkazi wa Kijji cha Wiri Wilayani humo,amesema Wiki hii Mei 5 ,29,2026,Tembo wamevamia shamba lake la Maharage na eneo la Nyumba moja na kumtia hasara kubwa,hivyo kuomba Serikali kuangalia kwa jicho la huruma kwani wanatumia gharama kubwa katika kilimo na mwisho wa siku wanaambulia patupu.

Habari Picha 17984

Hivi karibuni wakulima wa shamba la leoni wameamua kujingishana fedha kwa ajili ya kuweka watu wa kuwalindia mazao yao shambani,ambapo ulinzi huo umeanza kwa lengo la kunusuru chakula ili waweza kupata mazao mengi

Ambapo mwenyekiti wa wakulima upande wa ulinzi Muhamed Mzava,aliomba Maafisa wanyamapori kuwapa elimu watu hao waliochaguliwa kwa ajili ya ulinzi namna ya kuwadhibiti wanyama hao akiwamo Tembo wasiingie kwenye mashamba hayo ya wakulima

 

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment