Geofrey Stephen Arusha .
Arusha Mkurugenzi Mtendaji wa The Picnic Lounge jijini Arusha, Anthony Urasa, mapema leo amejumuika na wafanyakazi wake katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi). Tukio hilo lilijaa furaha na bashasha, huku wafanyakazi wakionyesha mshikamano na kufurahia uwepo wa kiongozi wao katika siku hii muhimu.

















