MGOMO WA WAKUSANYA MAPATO YA MAEGESHO WAKITA JIJI LA ARUSHA.

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Geofrey Stephen Arusha .

Jiji la Arusha leo, Septemba 30, limekumbwa na mgomo wa wafanyakazi wapatao 70 wanaokusanya mapato ya maegesho ya magari, ambao wamegoma kufanya kazi wakidai mishahara ya miezi miwili pamoja na mikataba rasmi ya ajira.

Wafanyakazi hao wanailalamikia kampuni ya Rick Plan Co. Ltd, wakidai kuwa wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu na chini ya masharti wanayoyataja kuwa ni magumu, huku wakisema hawana mikataba rasmi ya ajira.

Habari Picha 21514
Habari Picha 21512

Aidha, wafanyakazi hao wanadai kuwepo kwa malimbikizo ya michango ya NSSF kwa takribani miaka miwili, na wameitaka Serikali kuingilia kati ili kutatua changamoto hizo.

Wafanyakazi hao pia wanahoji uamuzi wa Jiji la Arusha kuipa kampuni hiyo tenda ya ukusanyaji wa mapato, wakitaka mamlaka husika kuchunguza uwezo na utendaji wa kampuni hiyo katika kutekeleza majukumu yake.

WADAI KULAZIMISHWA KUANDIKA MAGARI ZAIDI YA 300 KWA SIKU

Wafanyakazi hao wamedai kuwa wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu, huku wakilazimika kuandikia magari zaidi ya 300 kwa siku katika ukusanyaji wa mapato ya maegesho.

 

Habari Picha 21515
Habari Picha 21516

Mmoja wa wafanyakazi hao amesema:

“Tunafanya kazi katika mazingira magumu sana, jua kali na mvua, lakini mpaka sasa hatuna mikataba ya kazi. Kuna malimbikizo ya NSSF, na pia usipofikisha lengo unanyang’anywa mashine ya kukusanyia mapato. Huu ni unyanyasaji mkubwa sana kwetu.

“Wafanyakazi hao wanadai kuwa wananyanyasika kutokana na mazingira ya kazi, kutolipwa mishahara kwa wakati, kutokuwa na mikataba ya ajira na changamoto wanazodai kukumbana nazo katika ukusanyaji wa mapato,,

Wafanyakazi hao wamesema hali hiyo imekuwa ikiathiri maisha yao kwa kuwa wana familia zinazowategemea kwa mahitaji mbalimbali, yakiwemo chakula, malazi, ada za watoto na mahitaji mengine ya kifamilia.

Habari Picha 21518
Habari Picha 21517

Wameiomba Wizara yenye dhamana ya Kazi na Ajira pamoja na mamlaka nyingine husika kuingilia kati na kuchunguza madai yao, ikiwemo suala la mishahara, mikataba ya ajira na michango ya NSSF.

 

Habari Picha 21519

Mwisho.

Share This Article
Leave a Comment