πŸ”₯ AFCON ARUSHA YAPAMBA MOTO! Mwigulu Nchemba AAMURU UJENZI UFANYIKE SAA 24.

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Geofrey Stephen . Arusha

Kasi ya maandalizi ya miundombinu ya michuano ya Africa Cup of Nations 2027 imeingia katika hatua mpya baada ya Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, kutoa agizo kali kwa mkandarasi kuhakikisha ujenzi wa barabara za kuelekea uwanja wa AFCON jijini Arusha unafanyika mchana na usiku bila kusimama.

Ziara hiyo ya kushtukiza iliyofanyika Aprili 17, 2026 imelenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja pamoja na miundombinu yake, huku presha ikiongezeka kutokana na ujio wa wakaguzi kutoka Confederation of African Football wanaotarajiwa kuwasili hivi karibuni.

Habari Picha 17223
Habari Picha 17222

Ingawa baadhi ya maeneo yanaonesha mafanikio, Waziri Mkuu hakusita kueleza wazi kuwa kasi ya ujenzi wa barabara bado iko chini ya kiwango kinachohitajika.

β€œHakuna kusimama β€” kazi iendelee saa 24.

Ongezeni wafanyakazi, vifaa na juhudi mara moja,” alisisitiza kwa msisitizo mkali.

⏱️ Muda Wabana, Serikali Yachukua Hatua Kali.

Kwa mujibu wa maagizo hayo, barabara hizo zinapaswa kukamilika kabla ya Mei 2026, ikiwa ni sehemu ya maandalizi muhimu ya mashindano hayo makubwa ya bara Afrika.

Habari Picha 17224
Habari Picha 17225

Waziri Mkuu pia alionya kuwa ubora wa kazi haupaswi kuathiriwa kwa kisingizio cha kukimbizana na muda, akitaka viwango vya kimataifa viheshimiwe kikamilifu ili kulinda hadhi ya nchi wakati wa ukaguzi.

🚨 CCTV NA ULINZI WA KISASA WAINGIA MJINI.

Mbali na ujenzi, Serikali imeelekeza kuwekwa kwa mifumo ya kisasa ya ulinzi ikiwemo kamera za CCTV katika maeneo yote ya uwanja na viwanja vitakavyotumika.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha usalama wa mashabiki, wachezaji na wageni wa kimataifa pamoja na kudhibiti vitendo visivyofaa wakati wa mashindano.

⚠️ ONYO KALI KWA WAKANDARASI WAZEMBE.

Katika msimamo mkali, Waziri Mkuu alionya kuwa wakandarasi watakaochelewesha miradi au kushindwa kulipa wafanyakazi hawatavumiliwa na wataondolewa kwenye miradi ya Serikali.

πŸ‡ΉπŸ‡Ώ MAENDELEO YA TAIFA YAONGEZA KASI.

Akihitimisha ziara yake, alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuharakisha maendeleo ya taifa, akieleza kuwa dira mpya ya maendeleo na maboresho ya elimu ni hatua kubwa yenye mwelekeo wa kihistoria, akilinganisha na enzi za Julius Kambarage Nyerere.

Habari Picha 17226
Habari Picha 17227
Habari Picha 17228

Mwisho.

Share This Article
Leave a Comment