Na Mwandishi wa A24tv.
Rais wa Samia Suluhu Hassan ametangaza kwa masikitiko kifo cha Mbunge wa Jimbo la Isimani na aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi, William Vangimembe Lukuvi, kilichotokea leo Machi 25, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Lukuvi amefariki dunia majira ya saa moja asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Hospital, Jijini Dodoma, alipokuwa akipatiwa matibabu kufuatia ugonjwa wa mshtuko wa moyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa marehemu alikuwa pia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), na kifo chake ni pigo kubwa kwa serikali na wananchi wa Jimbo la Isimani.
Rais Samia ametoa pole kwa Spika wa Bunge, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki, pamoja na Watanzania wote kwa msiba huo mzito.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Moses M. Kushuka, ambaye amesisitiza kuwa serikali inaungana na familia katika kipindi hiki cha maombolezo.
Mwisho ..

