DED,SIHA ,AMETOA WITO KWA WANANCHI KUJITOKEZA KUOMBA MAOMBI YA MIKOPO YA ASILIMIA 10
KATIBU WA CCM SIH,ASISITIZA UMUHIMU WA MAREJESHO YA MIKOPO YA HALMASHAURI
Siha,Vikundi vinavyo pewa mkopo wa aslimia 10 za fedha za Halmashauri ya Siha mkoa wa Kilimanjaro wakiwamo vijana ,wanawake na Walemavu wametakiwa kutokubadili matumizi ya fedha hizo ili kufikia malengo waliyokusudia ya kuwaletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla
Haya yamesemwa leo March 6,2026,na Katibu wa CCM,Wilayani humo,Endrew Gwaje,wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani,ambapo Kiwilaya ilifanyika katika ukumbi wa Rc,Sanya juu
Akizungumza katika maadhimisho hayo,yenye kauli mbio haki na usawa kwa wanawake na wasichana msingi jumuhishi kufikia dira 2050, niwapongeze wale kina mama waliopata hizo fedha na vikundi vingine kama Vijana na walemavu,kama nilivyosema kikubwa ni kusisitiza marejesho.


Gwaje amesema ili muweze kukopa mara kwa mara ni kurejesha fedha hizo kwa wakati,ili kina mama wengine waweze kukopa ,hapa ndipo panapo kuwa na changamoto ambapo wengi hawarejeshi
“Niombe sana mfanye yale mlio kusudia kama ni miradi ya kufuga kuku mnaenda kufanya fanyeni ,ili muweze kurejesha na kina mama wengine waweze kupata hizo fedha kwani wengi wanahitaji”amesema Gwaje
Nimpongeze Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri hii,Hellen Mwambeta kwa kutenga fedha nyingi zaidi ya sh,300 milion ,kwa ajili ya Vikundi ,hongera kwa hilo,pia ni utekelezaji wa ila ya CCM,


Aidha amevitaka vikundi vinavyotaka kuchukua hizo,zile asilimia 10 ya mapato ya ndani ,timizeni vigezo,kwa hiyo niwaomba kina mama mchangamkie frusa hiyo sio kulia lia uko mtaani
Awali Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Hellen Mwembeta,ametoa wito kwa watu wote wenye sifa ,kundi la wenye ulemavu kundi la Wanawake na vijana ,waombe mikopo ,zaidi ya sh,300 milion fedha zipo na jukumu lao ni maombi
MKuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka,amewataka jamii Wilayani humo kutoa ushirikiano dhidi ya matendo ya ukatili wa kijinsia
Timbuka amesema takwimu zipo juu sana ,kwa sababu matukio yaliyoripotiwa kwa mwaka huu ni matukio 1076,ni matukio mengi sana kwenye wilaya yenye wakazi laki moja na arobaini
Amesema kuwa Mkaguzu wa polisi ametueleza vizuri sana ,kikubwa ambacho nawasii msificho uovu haya kwenye jamii zetu,bila kutoa taarifa ukatili huu na ukandamizaji utaendelea ,

kumekuwa na changamoto wanapofanyiwa ukatili wanapokuja kituo cha Polisi maelezo yanabadilika na yule mashuhuda muhimu wanageuka ,kesi inakosa udhahidi ,hatimaye kesi nyingi zinapotezwa au zinashindwa ni kutokana na kukosabushirikiano kutoka kwenye jamii
Naomba niwasihii linapokuja swala la kutoa ushikiano kwenye vyombo usika ikiwamo polisi na mahamani basi tutoe ushirikiano ili kukomesha matendo hayo,,vila ushirikiano ni kazi bure matukio yataendelea kuwepo
Mwisho

