TEA YAJA NA SULUHISHO KWENYE SEKTA YA NISHATI.

Geofrey Stephen
2 Min Read

Na Mwandishi wetu

Mwakilishi wa Wizara ya Nishati, Emilian Nyanda, amewapongeza wataalamu na wadau wa sekta ya nishati kupitia Tanzania Energy Association (TEA) kwa mchango wao mkubwa wa kuwaunganisha wadau wa nishati nchini.

Nyanda amesema hayo leo Februari 27, 2026, jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Karimjee, wakati wa hafla ya uzinduzi wa chama hicho. Amesitiza kuwa TEA ni jukwaa muhimu litakalosaidia kuunganisha nguvu za wananchi na wadau wote wa nishati kwa lengo la kusukuma mbele maendeleo ya sekta hiyo.

“Tunawapongeza TEA pamoja na wananchi wote kwa kuanzisha jukwaa hili muhimu. Kupitia TEA, imekuwa rahisi kwa Serikali kuwasiliana na wadau, kwani chama hiki kinaunganisha mawazo ya wadau na kuchukua ujumbe wa Serikali, badala ya Serikali kufuata mdau mmoja mmoja,” amesema Nyanda.

Habari Picha 7697

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TEA, George Michael, amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa chama hicho ni kuwaunganisha wadau wa nishati na kuwafanya kuwa sauti moja itakayowezesha kuwasilisha hoja, changamoto na mapendekezo yao kwa ufanisi, kabla ya kuwasilishwa kwenye wizara husika kwa ajili ya utekelezaji wa sera na sheria.

“Tunawakaribisha wadau wote na vyama mbalimbali vya nishati kuungana nasi, kushirikiana kwa karibu na kuangalia namna bora ya kusukuma gurudumu la maendeleo ili kufikia matumizi makubwa na bora ya nishati, hususan nishati safi inayohitajika sana katika jamii kwa sasa,” amesema George.

Aidha, George ameogeza kuwa TEA itakuwa msaada mkubwa kwa wadau wa nishati katika masuala ya kisheria, akieleza kuwa wadau wengi hukumbana na changamoto mbalimbali lakini hukosa mwongozo wa wapi pa kuelekea kupata msaada unaostahili.

Habari Picha 7697

Amesema TEA pia itawaunganisha wanachama wake na fursa za kimataifa kupitia ushirikiano, nchi na taasisi mbalimbali duniani, jambo litakalowezesha kubadilishana uzoefu na teknolojia. Kupitia chama hicho, wadau wanaojihusisha na uzalishaji na matumizi ya nishati kama gesi ya magari, petroli, oksijeni, biogesi, umeme wa maji (hydro) pamoja na taasisi kama Tanzania Atomic Energy Commission, watanufaika na mtandao mpana wa ushirikiano na maendeleo.

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment