WAZIRI MKUU Mwigulu Lameck Nchemba AKAGUA UJENZI WA STENDI KUU ARUSHA, MRADI WA BILIONI 14.3 WAFIKIA ASILIMIA 49

Geofrey Stephen
1 Min Read

Na Geofrey Stephen Arusha .

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, leo Jumanne Februari 24, 2026, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani katika Jiji la Arusha. Mradi huo unatekelezwa katika eneo la Bondeni City, mkoani Arusha.

Mradi wa stendi hiyo kuu unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 14.3 hadi kukamilika kwake. Lengo kuu ni kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, pamoja na kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji hilo linalokua kwa kasi.

Habari Picha 7348
Habari Picha 7347

Kwa mujibu wa taarifa ya wasimamizi wa mradi, hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 49, huku ukitarajiwa kukamilika mwezi Mei 2026.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi, Mhe. Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Gabriel Makalla.

Habari Picha 7349
Habari Picha 7350
Habari Picha 7351
Habari Picha 7352

Kukamilika kwa mradi huu kunatarajiwa kuleta mapinduzi katika sekta ya usafiri mkoani Arusha, kuongeza ufanisi wa huduma za mabasi yaendayo mikoani na kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika jiji hilo na maeneo ya jirani.

Mwisho ……

Share This Article
Leave a Comment