Na Bahati Siha.
Mbunge Mollel,aomba gari kwa ajili ya Kulinda mazao ya wakulima
Siha,Waziri mkuu wa Tanzania Mwingulu Nchemba ,ametoa pongenzi kwa Uongozi wa Hospital maalumu ya Taifa ya magonjwa yasiyoambukiza ya Kibong’oto kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa jengo la utawala
Haya ameyasema hayo leo February 21,2026, wakati wa ziara yake ya kikazi wilaya ya Siha mkoani hapa ,alipotembelea Hospital hiyo na kuweka jiwe la msingi kwenye jengo hilo


Akizungumza na viongozi mbali mbali wa Serikali,Dini pamoja na Wananchi waliofika katika eneo hilo,na kuwapongezi kwa kuonekana dhamani ya fedha katika ujenzi huo
“Nimekuja kujionea mradi wa ujenzi huu,jengo la utawala ,niwapongeze viongozi kwa kazi nzuri ,ambayo imefanyika ,jengo hili linaenda kwa kasi inayotakiwa ,mpo makini hakuna ubabaishaji”amesema Mwigulu
Mwigulu amesema kwenye ziara ,na makusudio ya ziara ni kukagua maendeleo ,kukwamua pale palipo kwama na kuchukua hatua mbali mbali kwenye maeneo yanayoitaji kuchukuliwa hatua
Amesema kwa kazi hii ambayo mmefanya vizuri ,ndiyo maana nimezindua uwekaji wa jiwe la msingi kama ratiba ilivyokuwepo
Pia ametoa angalizo kwa watumishi wanaofanya kazi kwa wazembe kwa mafufaa yao Serikali haita mvumilia ,sisi tushughulika na wale wote wanaofanya kazi kwa uzembe ,hatatusita kuwachukulia hatua
Awali katika taarifa yake Mkurungenzi wa Hospital hiyo Dkt ,Leonard Subi ,amesema matarajio ya Hospital ,kuwa taasisi inayojitegemea kisheria chini ya Wizara ya Afya ambapo mchakato wake unaendelea
Ambapo hadi kufikia may 1 ,2026,jengo hilo liwe limeanza kutumika na gharama ya ujenzi ni sh,3.9 bilion,Aidha amesema manufaa ni kuiweka taasisi na Nchi katika ramani ya tafiti za kibobezi Duniani
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo,Godwin Mollel,amemuomba Waziri wa mali asili na utalii Ashatu Kijaji, kupata magari mawili kwa ajili ya kusaidia kulinda mzao ya wakulima dhidi ya wanyama wanaoharibu mazao ya wakulima wakiwamo Tembo.


“Dada yangu wa Mali asili na utalii ,nisaidie kupata magari mawili sio mapya ,kwa ajili ya ulinzi wa wanyama wanaoharibu mazao ya wakulima wakiwamo Tembo “amesema Mollel
Amesema kuna Wakulima wa mashamba mbali mbali yakiwamo ya Leon na Pongo ,wamekuwa na hiyo shida ya mazao yao kuharibiwa na Wanyama kwa muda mrefu ,hivyo kuwasababishia kupata hasara kubwa na wakati mwingine kulazimika kununua chakula ili kukidhi mahitaji ya familia baada ya mazao yaonkuhatibiwa,jambo ambalo sio nzuri na la kukatisha tamaa
Mwisho



