MIAKA YA MABADILIKO: SERIKALI YAKAMILISHA MIRADI 81 YA BARABARA YA THAMANI YA SH BILIONI 500

Geofrey Stephen
3 Min Read

Na Geofrey Stephen Arusha .

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kuboresha miundombinu ya barabara nchini, baada ya kukamilisha jumla ya miradi 81 ya ujenzi na ukarabati yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 500.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku 100 za mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya ujenzi, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesema miradi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha usalama wa barabara na kuchochea shughuli za kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Habari Picha 6748

Fedha na utekelezaji wa miradi.

Kwa mujibu wa Waziri Ulega, Wizara ya Ujenzi imepokea jumla ya Sh bilioni 511 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo. Kati ya fedha hizo, Sh bilioni 280 zilitolewa na Hazina ya Serikali huku Sh bilioni 222 zikitokana na wahisani wa maendeleo.
Ameeleza kuwa Sh bilioni 125 kati ya fedha zilizotolewa na Hazina zimeelekezwa kwenye Mfuko wa Barabara, lengo likiwa ni kuwalipa wakandarasi wadogo.

wanaotekeleza miradi ya barabara katika maeneo mbalimbali nchini.

Miradi iliyokamilika na faida kwa wananchi.

 

Habari Picha 6750

 

Habari Picha 6749

Katika miradi hiyo 81, jumla ya miradi 40 imekamilika kwa asilimia 100. Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa King’ori, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, ulihusisha ujenzi wa daraja pamoja na uwekaji wa taa 136 za barabarani.
Waziri Ulega amesema mradi huo umeondoa changamoto kubwa ya usalama, hususan wakati wa mvua, na kuleta faraja kwa wakazi wa eneo hilo.

“Uwekaji wa taa za barabarani umeongeza usalama na umechochea shughuli za kiuchumi nyakati za usiku, hasa kwa wafanyabiashara wadogo,” amesema.

Uwajibikaji wa watendaji wasisitizwa
Akigusia suala la uwajibikaji,

Waziri Ulega amesema katika safari yake ya kukagua miradi ya barabara kutoka Dodoma, alikumbana na foleni kubwa ya malori katika mizani ya Mikese mkoani Morogoro. Baada ya uchunguzi, ilibainika kuwa foleni hiyo ilisababishwa na uzembe wa baadhi ya watendaji, hatua zilizochukuliwa mara moja kurekebisha hali hiyo.

Habari Picha 6752
Habari Picha 6753

Serikali imeendelea kusisitiza uwajibikaji na ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu, ili kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavyo na miradi inaleta manufaa ya moja kwa moja kwa.

 

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dk. Charles Msondo, amesema siku 100 za uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, zimeleta tija kwa wananchi na kuchangia kuinua uchumi wa taifa.

 

Mwisho.

Share This Article
Leave a Comment