THRDC NA MAIPAC yawanoa waandishi wa Habari za mazingira

Geofrey Stephen
3 Min Read

Mwandishi wetu,Arusha.

Mtandao wa watetezi wa haki za binaadamu Tanzania(THRDC) kwa kushirikiana na Taasisi ya wanahabari ya kusaidia jamii za asili(MAIPAC),imeanza kuwanoa wanahabari Kanda ya Kaskazini na Kati, kuandika vyema Habari za uchunguzi za mazingira.

Uzinduzi wa mafunzo hayo, umefanyika leo Februari 5,2026 jijini Arusha, kwa kushirikisha waandishi 35 kutoka mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Tanga, Singida,

Habari Picha 6668

Manyara na Dodoma na yanadhaminiwa na shirika la Umoja wa mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO).

Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa programu na uendeshaji wa THRDC, Wakili Halima Sonda, alisema wanahabari wanajukumu kubwa la kuhakikisha dunia na wananchi wanakuwa salama.

Habari Picha 6669
Habari Picha 6670

Wakili Sonda alisema Dunia inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira, hivyo wanahabari wanajukumu la kuokoa dunia na wananchi.

“lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wanahabari kuandika vyema Habari za mazingira, uchafuzi mazingira, ukataji miti na uchimbaji holela wa madini”alisema.

Akitoa mada juu ya uandishi wa Habari za mazingira katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa MAIPAC,Mussa Juma alisema ni muhimu wanahabari kujikita kuandika vyema Habari za mazingira kwani zina mahusiano makubwa na haki za binaadamu.

Habari Picha 6675

Juma alisema THRDC na MAIPAC inakusudia kutoa mafunzo kwa wanahabari 140 nchi nzima kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi, ukataji miti, uchafuzi wa mazingira, kudhibiti taka ngumu na masuala ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori na sheria mbalimbali za mazingira na ardhi.

“Baada ya mafunzo haya tunaimani tutakuwa na timu ya waandishi waliobobea katika masuala ya uandishi wa mazingira”alisema.

Juma alisema kuna Habari nyingi zinahitaji uchunguzi, ikiwepo umuhimu matumizi ya nishati safi na kuachana na kukata miji, uvamizi wa watu maeneo ya jamii za asili kama Wahadzabe na kufungua mashamba,uchimbaji holela wa migodi na matumizi ya kemikali zenye madhara, kusagaa kwa taka ngumu.

Habari Picha 6671
Habari Picha 6672

Akitoa mada ya sheria mbali mbali za ardhi, mazingira na Habari, Wakili Paulo Kisabo alisema, masuala ya mazingira yanauhusiano mkubwa na haki za binaadamu.

Kisabo alikumbusha wanahabari sheria mbali mbali za kimataifa na ndani ya nchi kuhusiana na masuala ya haki za binaadamu, mazingira na uhuru wa kujieleza.

“Wanahabari fanyeji kazi kwa kuzingatia sheria,mnalindwa na sheria nyingi za ndani na hivyo mkitumia vizuri kalamu zenu mtalisaidia sana taifa”alisema

Wakili Kisabo,alisema ni muhimu wanahabari kujua sheria mbali mbali kwa manufaa yao kwani kujifunza sheria sio kwa wanasheria pekee.

Habari Picha 6673
Habari Picha 6674

Mafunzo hayo, yanaendelea jijini Arusha na baadae yatafanyika katika kanda nyingine hapa nchini.

MWISHO.

Share This Article
Leave a Comment