WAKULIMA WA NAPILUKUNYA WALIA: HATUJAVAMIA ARDHI, TUNADAI HAKI YETU YA KISHERIA

Geofrey Stephen
5 Min Read

Na Mwandishi wa A24tv kiteto

Kwa muda mrefu sasa, wakulima wa eneo la Napilukunya, Wilaya ya Kiteto, wamekuwa wakikabiliwa na hali ya sintofahamu, vitisho na kunyimwa haki zao za msingi za kumiliki na kutumia ardhi waliyoipata kihalali. Kinachotokea kinatufanya tujiulize: je, serikali inatutambua kama raia halali au kama wavamizi wa ardhi yetu wenyewe?

Tulipata Ardhi Kihalali.

Wakulima wa Napilukunya hatukuamka tu na kuingia eneo fulani. Ardhi tuliyonayo tulinunua kwa mikataba halali kutoka kwa wenyeji, wakiwemo Akie (Wandorobo). Kama kuna hoja ya kujiuliza ardhi hiyo ilitokaje mikononi mwao, basi waliotuuzia ndio waliopaswa kuulizwa kwanza — si sisi wanunuzi wa halali.

Habari Picha 5863
Habari Picha 5864

Wengi wetu tuna mikataba ya manunuzi, wengine tuna hati za kimila. Hatujavunja sheria wala hatujavamia eneo la mtu.
Ahadi ya Serikali na Kuvunjwa kwa Matarajio.

Tarehe 29.12.2025, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto alikutana na wakulima na akaahidi kuwa ndani ya wiki moja, angepeleka wataalamu kuchunguza eneo lote la Napilukunya kwa mujibu wa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi wa 2015–2025, ili kubainisha:

Eneo la kilimo na makazi liko wapi
Eneo la malisho liko wapi

Alieleza wazi kuwa baada ya uchunguzi huo, angeweza kutoa tamko la haki na lisilo na upendeleo.

Hata hivyo, baada ya wiki kupita, DC aliandika barua akiahidi kukutana na wakulima na wafugaji tarehe 14.1.2026 kutoa tamko — jambo ambalo halikutokea kwa madai ya dharura. Baadaye, aliahidi tena mkutano tarehe 17.1.2026 katika.

Maktaba ya Kibaya.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Habari Picha 5867
Habari Picha 5869

Badala ya kutoa majibu ya tume zote mbili (yake na ile ya wataalamu wa wizara), aliahirisha tena akidai Mkuu wa Mkoa ndiye atatoa tamko tarehe 21.1.2026.

Amri za Kisheria.

Kinachoumiza zaidi ni kwamba wakulima waliamriwa kusimama mashambani mwao na mikataba yao kana kwamba ni wezi au wavamizi. Hili halikubaliki kabisa kisheria.
Hakuna mtaalamu wala kiongozi wa kiutawala mwenye mamlaka ya kumuamrisha mtu aache kutumia mali yake. Ni Mahakama pekee yenye uwezo huo.

Wakati huo huo, wafugaji wamepewa nafasi ya kuzuia trekta zetu zisiingie mashambani kulima, huku polisi wakitumwa kila tulipojaribu kuendelea na shughuli za kilimo, kwa madai kuwa “DC bado hajatoa tamko”.

Haya yote yanatuacha tukipoteza msimu wa kilimo bila hatia yoyote.

Eneo la Malisho Lipo Wazi.

Kitu kinachoshangaza ni kwamba eneo la malisho linajulikana na lina mipaka yake wazi, likiwa upande wa kaskazini mwa Enguseroandare, eneo linalomilikiwa na ndugu Pasinai Oltingi lenye zaidi ya ekari 6,000.

Swali letu ni moja:

Habari Picha 5872

Kama wafugaji wanahitaji malisho, kwa nini hawaonyeshwi eneo lao halali badala ya kudai mashamba ya wakulima?
Tulitegemea serikali iwe wazi kuwa:
Napilukunya ni eneo la makazi na kilimo
Malisho yako eneo la kaskazini, si mashambani kwetu.

Ramani na vipimo vya ardhi vipo sahihi. Sisi ni Watanzania halali, si wageni wala wavamizi.

Harufu ya Siasa na Mpango wa Kupora Ardhi.

Kwa masikitiko makubwa, tunajua kuna mpango unaosukumwa kisiasa wa kubadilisha mashamba yetu yawe malisho. Mpango huu unahusishwa na Mbunge wa Jimbo na Diwani wa Kata ya Partimbo, jambo ambalo hata wafugaji wenyewe wamelisema wazi.

Kama serikali inaamini tumekosea, basi ifungue kesi ya ardhi. Tuko tayari kusimama mahakamani. Lakini kuendelea kutupotezea muda wa kilimo ni dhuluma ya wazi.

Hatuko Tayari Kunyanyaswa Tena.

Mwaka jana, baadhi ya wakulima walifukuzwa mashambani mwao kama wahalifu na kushindwa kabisa kulima. Hili halivumiliki tena.
Wafugaji wanaodai mashamba si Akie, si wazaliwa wa Napilukunya, bali wanatoka:
Ngabolo
Ndedo
Nairero
Makame
Kilimbogo
Waliotuuzia ardhi wanajua wazi kuwa eneo hilo si malisho.
Hitimisho
Tunasisitiza tena:
Tulipata ardhi kihalali
Tuna mikataba na haki za kimila
Hatutaki upendeleo wala siasa
Tunataka haki na suluhisho la kisheria
Kama ni kesi — pelekeni mahakamani.
Kama ni haki — itendeni sasa.
Msitupotezee tena muda wetu .

Share This Article
Leave a Comment