Siha,
Wananchi wa kijiji cha Sanya juu,wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro,wameishukuru Serekali kwa kutoa fedha kiasi cha sh,94.9 , milion ,kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu 9 ya vyoo Shule ya Msingi Sanya juu Wilayani humo,ujenzi huo ni kutokana majengo ya shule hiyo kuwa chakavu
Kauli hiyo wameitoa leo junuar 10 ,2026,wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa huu,Nurdin Babu Wilayani humo kuangalia na kukagua miundombinu ya shule na maendeleo ya ujenzi wa vyumba hivyo vitatu katika shule hiyo ya msingi sanya juu hasa kipindi hiki cha kuelekea kufungua shule.


Wakizungumza wakati wa ziara hiyo ,Wananchi hao wamesema wanaishukuru Serikali kwa ujenzi huo kwani umekuja wakati muafaka kutoka na shule hiyo majengo yake kuwa ya siku nyingi na kuwa chakavu
“Ni kweli tunaishukuru Sarikali, kwani ujenzi umeanza wake umekuja wakati muafaka kwani vyumba vya madarasa vimekuwa chakavu ,hivyo kuwa tishio kwa wanafunzi wanasoma katika shule hiyo “Wamesema wananchi hao
Idrisa Mndeme mmoja ya wananchi wa eneo hilo,amesema kuwa shule hiyo ilijengwa miaka mingi liyopita ni kongwa,kutokana na hilo vyumba vyake vimechakaa sana hivyo kusababisha shule hiyo kuonekana kama gofu.


“Ujio wa haya madarasa matatu umeleta taswira ya shule kuonekana sasa,shule ni ya mijini hapa Sanya juu ,ilikuwa inatia aibu ,hivyo kuanza kwa ujenzi wa vyumba huu ni jambo nzuri,tunaishukuru serikali”amesema Idrisa
Aidha sambamba na hilo,drisa amesema anapenda kuiomba Serikali ya Mama Samia Suluhuu Hassan,hapo walipoanzia basi wasichoke kuongeza fedha kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa mengine yaliyobakia amesisitiza Idrisa
Kwa upande Mkuu wa mkoa huo,Nurdin Babu amesema hatua mliyofikia ya ujenzi ,sio hatua mbaya ,madarasa ni mazuri ,junuar 27,2026,takuja mwenyewe kuangalia kama jengo limekamilika,na hapa kila mmoja anawajibu wake ,kukaa ofisini hakuna tija sana,Engenia
Babu amesema Rais aneleta fedha nyingi kwenye nyanja mbali mbali ,Afya, Elimu,Barabara na maji,sasa anapoleta fedha hizi ,lazima kuhakikisha kwamba zinafanyiwa kazi kwa wakati.

Awali katika taarifa yake Mwalimu mkuu wa shule hiyo Beatrice Matela ,amesema kwa mujibu wa mkataba ujenzi wa vyumba hivyo,ulitarajia kukamilika Novemba 27,2025,
,lakini ulishindwa kukamilika muda kutokana na changomoto zilizojitokeza za mfumo wa manunuzi uliotokea Octobar ,2025,kusababisha kushindwa kununua vifaa vyavujenzi kwa wakati,hata hivyo ujenzi unatajia kukamilika junuar 27,2026
Mwisho



