MBUNGE WA PERAMIHO AFARIKI DUNIA, SPIKA AZUNGUMZA KWA HUZUNI

Geofrey Stephen
1 Min Read

MAREHEMU JENISTA JOAKIM MHAGAMA (23 Juni 1967 – 11 Desemba 2025)

Na Mwandishi wa A24tv Dodoma .

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), ametangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha Mbunge wa Peramiho, Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama, kilichotokea leo tarehe 11 Desemba 2025 Jijini Dodoma.

Akitoa taarifa hiyo Bungeni, Mheshimiwa Spika alisema:
“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kilichotokea leo 11 Desemba 2025 Jijini Dodoma. Natoa pole kwa Waheshimiwa Wabunge wote, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Peramiho. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.”

Spika ameongeza kuwa Ofisi ya Bunge, kwa kushirikiana na familia ya marehemu, inaendelea kuratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitatolewa kadri zitakavyokamilika.

Habari Picha 4705

Jenista Mhagama alikuwa miongoni mwa wanasiasa wanawake mashuhuri nchini, aliyewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini na ndani ya chama kabla ya kutumikia wananchi wa Peramiho kama Mbunge.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

 

Mwisho .

Share This Article
Leave a Comment