Serikali imekabidhi kiasi cha sh,1.2 bilion ujenzi wa kisasa soko la Masama mula.

Geofrey Stephen
4 Min Read

Na bahati Hai,

Serikali imekabidhi kiasi cha sh,1.2 bilion kwa ajili ya ujenzi wa Soko jipya la kisasa lilipo Masama mula Kata ya Masama mashariki Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro

Mradi huo umekabidhiwa Desembar 1 ,2025,lwa Mkandarasi , HUMPHREY CONSTRUCTION LTD ambapo matarajio ndani ya mwaka mmoja ujenzi wake utakuwa umekamilika.

Habari Picha 4604

Haya yanesema na David Lekei ,Afisa kilimo Halmshauri ya Hai kwa niaba ya Mkurungenzi mtendaji wa halmshaur hiyo,wakati wa akikabidhi mkataba wa ujenzi wa soko hilo kwa mkandarasi wa kampuni ya

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo,amewataka waliopewa dhima hiyo ya ujenzi nikuona mradi huo unakamilika kwa wakati ili wausika weweze kuanza kunufaika.

“Ni kweli leo Desembar 1 tumemkabidhi mkandarasi mkataba wa ujenzi wa Soko hili la Masama mula ,ambalo ni muhimu sana kwa huuzwaji wa bidhaa za kilimo mchanganyiko ikiwamo ndizi na maparachichi “amesema Lekei

Lekei amesema Serikali kupitia Wizara ya kilimo imekabidhi kiasi hicho cha fedha ,kwa ajili ya kuimarisha ujenzi wa soko la kisasa kabisa ,kwa sababu kipindi cha mvua katika soko hili kumekuwa na changamoto nyingi ikiwamo wafanyabiashara kunyeshwewa na mvua kusababisha matope soko nzima hapo.

Habari Picha 4606

Kutokana na hilo Serikali imeona ipo haja ya kulijenga soko hilo ili wafanyabiashara waweze kuuza bidhaa zao sehemu nzuri na wafanyabiashara wengine watavutika kuja kufanyabiashara katika eneo hilo na kuongeza kipato na kukuza uchumi wa eneo hilo

Kuleta Kessy mmoja ya mfanyabiashara wa soko hilo,amesema amesema anamshuru sana Rais Samia Suluu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa Masama mula

Soko hilo muhimu ambalo wanafanyabiashara ya bidhaa nyingi ikiwamo Ndizi,Parachichi mazao ya mboga mboga huuza bidhaa zao na kupeleka masoko ya mbali ikiwamo Dar esalamu ,Arusha na mikoa mingine

Ambapo amesema soko hilo limekuwa na changamoto hasa kipindi cha mvua ,zinaponyesha kunakuwa na adha ya uchafu wa aina mbali mbali ikiwamo matope kuzagaa sokoni hapo na hivyo kusababisha kero kwa wauzaji na wanunuzi wanaofika katika eneo hilo

“Ni kweli umechafuka matope mwili mzima kwa sababu ya kubeba ndizi na kuzipeleka sehemu nyingine,tunashukuru Mama samia kwani ujenzi huu umekuja wakati muafaka na ilikuwa ahadi ya muda mrefu tunashukuru “amesema Kuleta

Kwa upande wake Dismas Soka mkurungenzi wa kampuni hiyo,amesema anashukuru Serikali chini ya wizara ya kilimo ,ambapo amesema kwenye mradi huo,anachoomba ni ushirikiano wa pande zote kutoka Halmshauri ,Wizara pamoja na wananchi wa eneo hilo ili waweze kufanikisha jambo hilo

Awali Muhandisi wa ujenzi wa Wilaya Matandiko Arnold ,
anesema ,mwaka jana hoja ya ujenzi wa Soko liliibuliwa hapa na Wananchi wa hapa pamoja ma wafanyabiashara wa soko hili

Ambapo wataalamu walifika na kufanya tathimini kupima kuandaa michoro ya kila kitu ya namna soko hilo litakavyokuwa ,baada ya michakato mingi kupita ndiyo amepatikana mkandarasi ,hivyo leo amekuja kukabidhiwa mradi huu

Soko hili litajengwa kisasa kutakuwa na sehemu ya kuuzia ndizi ,maeneo ya watu wa chakula na vinywaji na chumba cha kuhifadhi mazao

 

Mwisho.

Share This Article
Leave a Comment