Na Mwandishi wa A24tv Dar es Salaam
Mahakama va Hakimu Mkazi Kisutu, Jiiini Dar es Salaam Leo Novemba 07, 2025, imewasomea mashtaka matatu (3) ya uhaini , Mfanyabiashara Jenifer Jovin (Niffer pamoja na wenzake 21
Kwa mujibu wa mashtaka valiyosomwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi. Clemence Kato mbele va Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya, kosa la kwanza ambalo linawakabili Washtakiwa wote 22, ni kosa la kula njama ya pamoja na kupanga uhalifu ambao ni uhain
Pia kosa la pili ambalo ni la uhaini linawahusu washtakiwa 21 isipokuwa mshtakiwa mmoja pekee ambaye ni Niffer, ambapo washtakiwa walianzisha nia ya kuzuia uchaguzi Mkuu 2025, na kutishia mamlaka na wakatekeleza nia hivo kwa kufanya vurugu zilizosababisha uharibifu wa mali za umma,
Aidha kosa la tatu la uhaini pia linamhusu mshtakiwa namba moja pekee ambaye ni Niffer, ambapo alihamasisha watu kuvuruga uchaguzi Mkuu 2025 na kuhamasisha umma kununua barakoa za kuzuia mabomu va machozi kutoka dukani kwake.
Mwisho .



