Luteni Kanali Meidin Apiga Kura, Atoa Wito wa Amani Katika Uchaguzi Mkuu 2025

Geofrey Stephen
1 Min Read

 

Na Geofrey A24tv .

Luteni Kanali Meidin (Mstaafu) wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, mapema leo ametimiza haki yake ya kikatiba kwa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Ikumbukwe kuwa Luteni Kanali Meidin alikuwa miongoni mwa waliotia nia kugombea ubunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi mwaka huu. Katika mchakato wa ndani wa chama, jina lake lilifanikiwa kuingia kati ya watia nia watano waliokuwa wakisaka ridhaa ya wajumbe. Hata hivyo, baada ya mchujo, jina la Dkt. Joanes Lukumay liliidhinishwa kuwa mgombea rasmi wa ubunge wa jimbo hilo.

Habari Picha 3846

Baada ya kupiga kura, Luteni Kanali Meidin alizungumza na waandishi wa habari na Watanzania kwa ujumla, akisisitiza umuhimu wa kudumisha amani, umoja na upendo katika kipindi hiki cha uchaguzi.

“Uchaguzi ni sehemu ya demokrasia. Ni muhimu tufanye kila kitu kwa amani, tusihatarishe umoja wetu kwa tofauti za kisiasa,” alisema Meidin.

Luteni Kanali Meidin alihitimisha kwa kuwataka Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura huku wakiheshimu maamuzi ya wengine na kuacha chuki au vurugu.

Mwisho .

Share This Article
Leave a Comment