Idadi ya Wananchi 150147 jimbo la Hai mkoa wa Kilimanjaro wanatarajia kupiga kura tarehe 29, wahakikishiwa usalama wao.

Geofrey Stephen
3 Min Read

Idadi ya Wananchi 150147 jimbo la Hai mkoa wa Kilimanjaro wanatarajia kupiga kura tarehe 29, wahakikishiwa usalama wao

Uku akitoa wito kwa wapiga kura ambao ni Wananchi kujitokeza kwa wingi ,kupiga kura ni tendo la kidemokrasia ili kupata viongozi watakaoshirikiana kuleta maendeleo

Hai,Wananchi 150147 wa jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro wanatarajia kupiga kura katika uchaguzi Mkuu unatarajia kufanyika Oktoba 29, Mwaka huu ,huku maandalizi yakiwa yamekamilika kwa asilimia mia ikiwa ni pamoja na uwepo wa vifaa vya kupigia kura.

Habari Picha 3816
Habari Picha 3817

Hayo ameyasema leo Jumatatu Oktoba 27, 2025 na Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro Aidan Angetile ,wakati akizungumza ma waandishi wa Habari ofisini kwake

‘Ni kweli natoa wito wangu kwa wapiga kura ambao ni wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga lura ,kwani haki yao ya msingi ili kupata viongozi wataoshirikiana nao kuleta maendeleo,kura yako ni muhimu’amesema Aidan

Aidan amesema wana vituo 406 katika kata 17 za jimbo hilo na tayari wameshatoa zoezi la kufundisha kwa makarani wa vituo watakao waongoza wananchi,aidha jana na leo zoezi la kuwafundisha wazimamizi wa vituo na wasaidizi wao linamalika leo

Amesema mbali na hilo pia wamefanya zoezi la kuwafundisha mawakala 124 kutoka vyama mbali mbali vya siasa kutoka jimbo hilo

Amesema mpaka sasa hali ni nzuri maendeleo yamekamilika kwa asilimia 98,asilimia 2 iliyobaki ni haya mafunzo yanayomalizika leo na usambazaji wa vifaa kwenda kwenye vituo

Ametaja kwamba katika jimbo hilo vyama vinavyoshiriki katika uchaguzi huo,ni CCM,Act wazalendo,NRA,Chauma,na Chama Makini

Wito wangu kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura, vifaa vyetu vimewasi na vya kupigia kura na sasa tunavisambaza kwenye vituo husika lakini pia usalama upo wa kutosha kwa kila atajayetoka kwenda kupiga kura siku ya tarehe 29,”

Kwa sasa taasisi mbali mbali wakiwamo Viongozi wa Dini wamekuwa wakiwaimiza wananchi kujitokeza kupiga kura kwani ni haki ya ya Misingi ya kupata viongozi watakao waletea maendeleo

SHaabani Mlewa Sheikh wa mkoa wa Kilimanjaro akiwa katika moja ya kikao na viongozi wa Dini wa mathehebu mbali mbali,ametaka viongozi hao kuendelea kuliombea Taifa kuendelea kuwa na amani na utulivu hasa wakati huu wakuelea kwenye uchaguzi mkuu

 

Mwisho .

Share This Article
Leave a Comment