JAMES MBOWE ATOA AHADI YA AJIRA KWA VIJANA ENDAPO ATASHINDA UBUNGE JIMBO LA HAI

Geofrey Stephen
3 Min Read

Na Mwandishi wa A24tv.

Hai,Wakati kampeni za vyama mbali mbali vya kisiasa zikiendelea ,Mgombea ubunge jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro kupitia cha cha Chauma Jemsi Mbowe, amesema pamoja na mambo mengine ameahidi kutumia Mlima Kilimanjaro kuongeza ajira kwa vijana wa jimbo hilo kupandisha Wageni katika mlima huo

Haya ameyasema wakati wa mkutano wa kampeni uliiyofanyika Kata ya Machame kaskani eneo la mfoni ,kuomba ridhaa ya kuongoza jimbo hilo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika October 29 ,2025.

Habari Picha 2888

Akizungumza na wananchi waliofika katika. mkutano huo wa kunadi sera za chama chake ,amesema Mungu amebariki kuwa na Mlima Kilimanjaro, ambao ni frusa nzuri ambayo inasaidia kuongeza ajira kwa vijana

#Ni kweli katika ahadi zangu moja wapo ni kuzalisha ajira kwa vijana wetu,kupitia lango la machame kupandisha Wageni kwenda mlima Kilimanjaro, baada ya kuona jambo hilo ni ftusa lakini vijana wa eneo hili hawapati#Amesema Mbowe

Mbowe amesema ,amelazimika kutoa ahadi hiyo,baada ya kubaini vijana wengi wapo mtaani ,hawana ajira wapo ,wakiishia kwenye vilevi ,huku frusa zipo za kupandisha Wageni katika mlima Kilimanjaro kupitia kampuni ambayo ipo katika eneo hilo ya Alteza

Amefafanua kwamba ,zamani kulikuwa na mashamba ya kahawa kama Kibohehe na mashamba mengine vijana wallikuwa wanapata ajira ya kuchuma kahawa ,lakini sasa imekuwa changamoto ,ajira hakuna tena ya kuchuma kahawa hivya kuwa na vijana wasiokuwa na matumaini.

Habari Picha 2889

Ndiyo sababu ya kusema kuwa kuna Kampuni ipo hapa Aishi ya Alteza inaongoza kwa kupandisha Wageni katika mlima huo ,lakini hapa kwetu vijana wangapi wananufaika na ajira hizo za kupabdisha wageni

Kwa mfano mkinichagua mimi nikawa Mbunge, tutaunda chama hapa cha vijana, kuna fedha za jimbo ,hizi tutazumiweka ,tutawafundisha hawa vijana wawe na ujuzi wa kuongoza Wageni

Kijana ambaye yup hapa kijijini hapa hafahamu kuongea lugha ya kiingereza atafundishwa kozi ya miezi mitatu ataongea kiingereza vizuri atachukua Wageni hapa na kupanda mlima Kilimanjaro

Tafsiri yake nini ni tukiunda kikundi hicho ,tukawajengea uweze vijana 100 na kuendelea ,nakuwafuata Kampuni kama ya Alteza ambao wamewekaza hapa kwetu,tunaomba zinapotokea ajira za kupandisha Wageni, basi waletewe kwenye chama Chao cha Nshara

Amesema mgeni mmoja anakuwa na wasaidizi watatu,akiwamo mpishi ,wakipanda mlima wanakaa mlimani kwa siku saba,akishuka hapa ana Dolla,ananunua nyama buchani,muuza nyama ananufaika na fedha za mpanda mlima,kwa ujumla hali ya kiuchumi ilikuwa nzuri kwa vijana

Aidha mgombea udiwani kupitia chama hicho, Nelson Massawe,ameahidi kutoa elimu kuhakikisha wananchi wanajengewa uwezo kabla kupewa fedha za mikopo ili waweze kurejesha kwa amani fedha hizo

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment