Siha,
Mgombea udiwani Kata ya Sanya juu Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro,kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Juma Jani,ameahidi kujenga Soko la Kisasa ili wafanya biashara waweze kufanya biashara zao katika mazingira salam
Jani ametoa ahadi hiyo leo Agost 30 ,2025,wakati wa kampeni ya kuomba ridhaa kwa Wananchi wa kijiji cha Merali kuongoza kata hiyo kwa mara nyingine tena
Ambapo amesema mengi yamefanyika kwenye kata hiyo, lakini anatambua bado kuna mengi yanahitajika kufanyika, ikiwamo wa baadhi ujenzi wa Barabara ndani ya kata hiyo .

Ni kweli ahadi yangu kubwa ,vipaumbele vyangu vikubwa ni pamoja na ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Merali ilikupunguza mrundikano katika Shule ya Sekondari Kilingi pamoja na ujenzi wa soko la kisasa Sanya juu #a.amesema Jani
Jani amesema kwa sasa asilimia 70 ya Wafanyabiashara wa eneo hilo ,Wanafanyabiashara bara barani ,kwenye mazingira kama hayo ni hatari kwao na kuufanya mji kuonekana katika mazingira yasiyopendeza,Hivyo linajengwa Soko linakuwa la siku zote ,
Pia amesema sambamba na hilo,katika jitihada zake amefanikiwa kupata eka tano kwa ajili ya ujenzi wa Gulio ,ambalo litakuwa kariba na Hospital ya Wilaya hiyo na kuongeza uchumi wa eneo hilo.


Idrsa Mndeme Meneja kampeni Akizungumza wakati akimnadi mgombea huyo ,katika kijiji cha Sanya hoyee,alikumbusha namna ya kukabidhiti tembo wanaoharibu mazao ya wakulima ,kwa kuweka vizuizi kwenye njia wanazopita ikiwamo kufunga taa,ambapo pia alishauri kuwepo uwanja wa michezo mzuri kwenye kata hiyo
Ni kweli tembo wamekuwa wakijaribu Mazao ya wakulima kwenya mashamba ya pongo na Leon kila ,mwaka bila ufumbuzi wowote hivyo tumeshauri njia wanapopitia kutoka msituni kuja kwenye mazao pawekwe kizuizi ikiwamo kufuga taa #amesema Idrsa .


Mbali na hilo Mgombea Ubunge wa jambo hilo la Siha,kupitia CCM, Goodwin Mollel ,anatajiwa kuzinduliwa kampeni September 6,2025,Sanya juu katika viwanja vya Rex,kuja kunadi sera zake
Mwisho