JOSHUA NASARI SINTAKUA MBUNGE WA POSHO NITALETA MAENDELEO KWA KASI SANA JIMBONI .

Geofrey Stephen
2 Min Read

Na Geofrey Stephen Arumeru

Mashariki Wananchi kutoka vijiji na kata mbalimbali walijitokeza kwa wingi kumsindikiza, wakiwa na nyuso za furaha, nderemo na vifijo. Barabara zilipambwa kwa rangi za kijani na njano, huku mabango yenye jumbe za matumaini na maendeleo yakibebwa kwa shangwe.

Usafiri wa helikopta uliotumiwa na Nasari uliendelea kunogesha tukio hilo na kuongeza hamasa kwa wafuasi wake.

 

Habari Picha 2255
Habari Picha 2256

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu, Nasari alisema kuwa safari ya maendeleo ya Arumeru Mashariki  imefika hatua mpya. Aliahidi kusimama bega kwa bega na wananchi katika kushughulikia changamoto sugu zinazowakabili, ikiwemo maji safi, barabara na huduma nyingine za kijamii.

“Huu ni wakati wa kuibadilisha Arumeru na kuifanya wilaya yenye matumaini mapya. Nitasimama mstari wa mbele kushirikiana na wananchi na viongozi wote kuhakikisha kila mmoja anafaidika na matunda ya maendeleo,” alisema kwa msisitizo huku akishangiliwa na wananchi.

 

Habari Picha 2251

Nasari pia aliwataka madiwani wa CCM kufanya kazi kwa bidii na mshikamano, akisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanahitaji mshirikiano wa pamoja.

“Sitakuwa mbunge wa posho, bali wa vitendo. Wananchi wa Arumeru wanahitaji matendo, si maneno matupu,” aliongeza.

Aidha, aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili kumchagua Rais, Mbunge na Madiwani kupitia CCM, akieleza kuwa chama hicho ndicho kinachoendelea kupeleka maendeleo kwa Watanzania.

 

Habari Picha 2257
Habari Picha 2258
Habari Picha 2259

Mwisho, Nasari aliwashukuru wananchi waliomsindikiza na kumuunga mkono, akiahidi kuwalipa imani hiyo kwa kushirikiana nao ili kuhakikisha ndoto ya maendeleo inafika kila kijiji na kila kaya.

Habari Picha 2260
Habari Picha 2261
Habari Picha 2262

Mwisho .

 

Share This Article
Leave a Comment