Na Bahati Hai,
Kamati ya lishe Halmashauri ya Hai mkoani Kilimanjaro ,imefanya kikoa cha robo ya kwanza kilichofanyika katika ukumbi wa Hospital hiyo na kujadili maswala mbali mbali ya ikiwamo lishe bora kwenye jamii pamoja na changamoto zilizopo
Hayo yamesemwa leo Novembar 12 ,2025 na Abel Mwaipungu Afisa lishe wa Wilaya hiyo na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wa maendeleo wakiwamo wakuu wa idara wa halmshauri hiyo.


“Ni kweli leo jumatano tumekuwa na kikao ,tumeweza kuzungumzia maswala ya lishe kwani lishe bora ndiyo msingi wa kujenga kizazi chenye afya njema ,pamoja na uchangiaji wa chakula shuleni “amesema Abel
Abel amesema mmoja ya mjadala waliokuwa wanajadili katika kikao hicho kwenye kamati hiyo ni kuwa namna gani ya kusaidia jamii kuweza kujizuia na magonjwa yasiyoambikiza ambalo ni tatizo linalokuja kwa kasi katika Nchi yetu
Amesema kizazi cha sasa kimeharibika na matumizi ya vyakula hivyo nakuomba kuwepo elimu kuepuka vyakula hivyo visivyokuwa na faida mwilini,wageukie vyakula vya asili ambavyo kwa kiasi kikubwa vina virutubisho muhimu kwa mwili wa binadamu
Amesema kupitia kamati hiyo,imeonekana ni jukumu la kila mtu kuhakikisha ,kwanza anaelewa na kutoa elimu ya lishe kwa wengine kuona umuhimu wa kula vyakula vya asili ili kujizuia kupata magonjwa hayo,yakuwamo shinikizo la damu na sukari,ambapo gharama ya kutibu magonjws hayo ni kubwa sana
Mbali na hilo pia wameomba wazazi kuwa na mwamko wa kuchangia chakula shuleni ili watoto wawezo kupata chakula , kwani kuna baadhi ya wazazi wamekuwa na utoro wa kutokuchangia , mtoto kikosa chakula shuleni sio jambo nzuri inaweza kusababisha kiwango cha elimu kushuka
Kwa upande wake mmoja ya wajumbe hao,Deogratius Sumar,amesema wamekubaliana katika kikao hicho, kutoa elimu kwa wafanyabiashara wanaokaaga chpsi na samaki kutotumia mafuta zaidi ya mara mbili ,kwa lengo la kutengeneza faida kubwa ,kwani ni hatari kwa afya.


Amesema kwa wafanyabiashara hao kutengeneza faida kunawaeza kuja tatizo la kuumiza wengine,watu wanaweza kupata magonjwa ya Moyo,Ini na madhara mengine ya kiafya mabaya sana ambayo yanahitaji gharama kubwa
Kitaalamu unapotumia yale mafuta zaidi ya mara mbili ,nini kinatokea kunatengenezeka kemikali ambazo zinakwenda kuasiri afya ya binadamu
Kwa hiyo tumekubaliana kuelimisha watu hao,ili waone umuhimu wa kutokutumia mafuta zaidi ya mara mbili kwa ajili ya kulinda afya ya walaji
Mwisho

