Shirika la FTK,lajikita kuchangia chakula shuleni ili kuboresha elimu.

Geofrey Steven
3 Min Read

Na Mwandishi wa A24tv Hai,

Shirika lisilo la Kiserikali la FTK,lilipo TPC mkoani Kilimanjaro limekuwa na program ya kuchangia chakula shuleni za maeneo mbali mbali kupunguza utoro pia mwanafunzi mwenye njaa huwa hafundishiki ukilinganisha na wanaopata chakula walau cha mchana

Haya yamesema na lemaibe Syokino Meneja miradi kutoka shirika hilo lililo na makao yake TPC,mkoani Kilimanjaro,wakati wa kuzindua huduma ya upimaji magonjwa mbali mbali bure kwa watoto kuanzia mwaka sifuri hadi miaka 9 ,katika Kijiji cha Mkarama Wilayani Hai mkoani hapa kwa siku tatu.

Habari Picha 21915

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo kufanyika Oktobar 21,2026 , amesema hatua ya kuwa na mpango wa kutoa chakula shuleni ni kwamba kile chakula kinachotolewa na Wazazi hakitoshelezi kama shirika wameona kuwa na utaratibu huo wa chakula ili kuboresha elimu

“Ni kweli kwa upande wa elimu tunaprogramu ya chakula shuleni ,kwamba kinachotolewa na wazazi wakati mwingine hakitoshi ,kwa hiyo kama shirika FTK,tumeona kuwashika mkono kuboresha elimu,watoto waweze kupata chakula cha kutosheleza “amesema Lemaibe

Amesema kuwapatia chakula shuleni ni sehemu ya utunzaji wa rasilimali watu na maandalizi ya kizazi chenye afya na uwezo wa kushiriki katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa.

Habari Picha 21916

Lemaibe amefanunu kwa kusema kwamba mwanafunzi mwenye njaa huwa hafundishiki ukilinganisha na wanafunzi wanaopata chakula ikiwamo chakula cha mchana

Awali katika taarifa yake amesema shirika hilo mbali na kutoa chakula mashuleni limeweka kambi ya Afya kuwahudumia watoto kuanzia umri wa mwaka sifuri hadi miaka tisa kwa kuwapa chanjo katika Kijiji hicho cha Mkarama

lakini pia kupima magonjwa kuhusiana na masikio magonjwa ya ngozi na wale watakatambulika kuwa na changamoto ya Afya nyingine tofauti watapelekwa Hospital ya TPC,na hata mara nyingine wanapelekwa Hospitali ya rufaa ya KCMC,wanakuwa wanasaidiwa bure na shirika hilo.

Habari Picha 21917

Mwenyekiti wa Kijiji hicho,Said Mushi ametoa shukurani kwa shirika hilo kwa kufanya kambi ya Afya kuhudumia watoto na watakaobainika kuwa na changamoto wanapatia matibabu , ni jambo jema na linatakiwa kuigwa ,kwani ni kuunga mkono juhudi za Serikali kusaidia jamii kuwa na Afya njema

Kwa upande wake Nsajigwa Ndagile Afisa Tarafa masama ambaye alikuwa mgeni rasmi,ameiomba jamii ya eneo hilo kuwaunga kwa kuwapa ushirikiano waone kwamba kitu walichopanga kwa ajili yao kinafanikiwa kwa ufanisi mkubwa.

Habari Picha 21918

“Ni kweli tuwaunge mkono ,tuwape ushirikiano kuhakikisha watoto wetu wanapimwa magonjwa mbali mbali watakaobainika wanachangamoto naamini watahudumiwa ,naomba sana tutoe  ushirikiano wakutosha,matibabu ni bure”amesema Nsajigwa

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment