WAZIRI KADOGOSA AAGIZA BARABARA ZA MBAUDA– KILOMBERO SOKONI NA ARUSHA BYPASS KUKAMILIKA KWA WAKATI.

Geofrey Steven
3 Min Read

Na Geofrey Stephen .ARUSHA,

Oktoba Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Massanja  Kadogosa, amemtaka Mkandarasi wa Kampuninya  China Railway Construction Engineering Group (CRCEG anayetekeleza ujenzi wa  sehemu ya Barabara ya Kisongo Kilombero  Sokoni kuhakikisha  kinajengwa kwa mujibu wa mkataba na kuzingatia viwango na ubora unaotakiwa.

Waziri Kadogosa ametoa agizo hilo  mkoani Arusha wakati akikagua miradi ya barabara inayotekelezwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa ajili ya maandalizi ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027. Ukaguzi huo umefanyika katika maeneo ya Mbauda, Mushono na Kwa Mromboo.

Habari Picha 21674
Habari Picha 21675
Habari Picha 21676

Akiwa Mbauda, Waziri Kadogosa amepongeza maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo, akieleza kuwa kilomita 13 zimepewa kipaumbele maalum katika maandalizi ya AFCON 2027. Kipande hicho kinajumuisha Mbauda–Arusha Bypass chenye urefu wa kilomita 7.4 na Tanganyika Packers–Kiserian chenye urefu wa kilomita 5.6, ambavyo vinatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2026.

Amesema anamfahamu Mkandarasi huyo kutokana na utendaji wake katika miradi mbalimbali nchini, hivyo anaamini atakamilisha kazi hiyo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

“Mkandarasi huyu si mgeni kwangu. Ninaamini atafanya kazi vizuri hapa kama ambavyo tumemuona kwenye miradi mingine ambayo anaitekeleza nchini,” amesema Kadogosa.

Habari Picha 21678
Habari Picha 21679

Aidha, amemtaka Mkandarasi kutumia mradi huo kama fursa ya kujenga rekodi nzuri ya utekelezaji na kuongeza nafasi ya kupata kazi nyingine za ujenzi wa barabara, kwa kuhakikisha anamaliza kazi kwa wakati, kwa ukamilifu na kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa.

Kwa upande wa TANROADS, Meneja wa Mkoa Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Arusha, Mhandisi Reginald Massawe wa amesema mradi  huo utasaidia  kuboresha usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla, pamoja na kurahisisha usafiri wakati wa AFCON 2027.

Amesema mradi huo pia unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kudhibiti maji, hatua inayolenga kutatua changamoto ya maji ambayo imekuwa ikisumbua maeneo hayo kwa muda mrefu.

Habari Picha 21680
Habari Picha 21681
Habari Picha 21682

“Tukikamilisha miundombinu hii ya maji, tunaamini tutakuwa tumepata suluhisho la kudumu,” amesema.

Meneja huyo amesema Serikali pia imeendelea kuhakikisha malipo ya fidia kwa wananchi wanaoathiriwa na utekelezaji wa mradi yanafanyika kwa wakati.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Paul Makonda, amesema matarajio yake ni kuona mradi huo unakamilika kwa wakati sambamba na kuwekwa kwa taa za barabarani, vituo vya mabasi na upandaji wa miti kwa lengo la kulipendezesha Jiji la Arusha.

Habari Picha 21683
Habari Picha 21684
Habari Picha 21685

Amesema miundombinu hiyo itasaidia kuboresha mazingira ya usafiri na huduma za kijamii, pamoja na kuongeza mvuto wa jiji kuelekea maandalizi ya AFCON 2027.

 

Mwisho…

Share This Article
Leave a Comment