Na Geofrey Stephen Arusha .


Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, Mrakibu wa Polisi (SP) Dkt. Sotery Flavian, amefika nyumbani kwa familia ya marehemu Daniel Lema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Safina Radio ya Jijini Arusha, kutoa salamu za pole na rambirambi kwa familia kwa niaba ya Jeshi la Polisi Arusha.
Akizungumza wakati wa kutoa pole, SP Dkt. Sotery Flavian ameeleza masikitiko yake kufuatia kifo cha Daniel Lema, akisema msiba huo ni pigo kubwa kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na watu mbalimbali walioguswa na maisha na mchango wake katika jamii.

Amesema Jeshi la Polisi Arusha limetambua uzito wa msiba huo na kuona umuhimu wa kufika pamoja na familia katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, kama ishara ya mshikamano, faraja na heshima kwa marehemu.
SP Dkt. Flavian ametoa pole za dhati kwa familia ya marehemu, huku akiwaomba kuwa na subira, uvumilivu na mshikamano katika kipindi hiki cha majonzi.
Aidha, ameeleza kuwa Daniel Lema alikuwa sehemu ya jamii ya Arusha na mchango wake kupitia Safina Radio ulifanya awe na nafasi muhimu katika maisha ya watu mbalimbali, hivyo kuondoka kwake kumeacha pengo kwa familia na jamii kwa ujumla.

Kwa niaba ya Jeshi la Polisi Arusha, SP Dkt. Sotery Flavian amewasilisha salamu za rambirambi kwa familia na kuwaomba waendelee kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki cha kuomboleza.
“Tunatoa pole za dhati kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Daniel Lema. Tunawaombea nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Jeshi la Polisi Arusha lipo pamoja nanyi katika wakati huu wa huzuni,” amesema SP Dkt. Flavian.



Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Daniel Lema mahali pema peponi na awape familia, ndugu, jamaa na marafiki nguvu na subira katika kipindi hiki cha majonzi. Amina.
Mwisho..
