DC, KARANGA ATEMBELEA ATHARI ZA MVUA ENDALA–CHEMCHEM, AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUREJESHA MIUNDOMBINU

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Geofrey Stephen  Karatu

Mkuu wa Wilaya ya Karatu, , ametoa maelekezo mazito kwa taasisi za serikali kuhakikisha hatua za dharura na za kudumu zinachukuliwa kurejesha miundombinu iliyoharibiwa na mvua kubwa katika Kijiji cha Endala–Chemchem.

Habari Picha 17010

Katika ziara ya ukaguzi iliyofanyika Aprili 10, 2026, DC Karanga alijionea uharibifu mkubwa wa barabara ya mzunguko (Bypass) inayounganisha Manyara Kibaoni, Endala hadi barabara ya Mbulu. Maeneo kadhaa yamekatizwa na mito, hali inayofanya usafiri kuwa wa hatari na usiotabirika.

Habari Picha 17006

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Karanga alisisitiza kuwa hali hiyo haiwezi kuvumiliwa na kwamba serikali imejipanga kuhakikisha mawasiliano ya barabara yanarejeshwa haraka ili wananchi waendelee kupata huduma muhimu bila vikwazo.

Katika ziara hiyo, aliambatana na wataalamu kutoka na pamoja na viongozi wa vijiji na wananchi wa eneo hilo. Kwa pamoja walikagua maeneo yaliyoathirika zaidi.

DC Karanga alieleza kuwa serikali imeanza mchakato wa kufanya upembuzi yakinifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa madaraja imara yatakayoweza kuhimili mvua na majanga ya asili, ili kuondoa kabisa changamoto ya kukatika kwa mawasiliano.

Habari Picha 17007

Alisisitiza kuwa suluhisho la kudumu ndilo linalohitajika, na kuiagiza TARURA kuharakisha hatua za kitaalamu zitakazopelekea utekelezaji wa miradi hiyo.

Aidha, alimwagiza Meneja wa TANESCO Wilaya ya Karatu kushughulikia changamoto za umeme katika vijiji vinavyopitiwa na mradi huo, akibainisha kuwa nishati ni muhimu katika kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Habari Picha 17008
Habari Picha 17009

Kwa upande wake, DC Karanga aliwataka wananchi kushirikiana na serikali kwa kulinda miundombinu na kutoa taarifa mapema pale wanapoona dalili za uharibifu.

Akihitimisha ziara hiyo, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, , kwa juhudi za kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara kupitia TARURA, akieleza kuwa hatua hizo zinafungua fursa mpya za maendeleo kwa wananchi wa vijijini, hususan Wilaya ya Karatu.

Mwisho….

Share This Article
Leave a Comment