Na Richard Mrusha A24TV
Serikali imeeleza kuwa uwekezaji wa halal (Halal Investment) ni miongoni mwa fursa zinazoweza kutumika kuvutia mitaji kutoka nchi za Mashariki ya Kati na Asia, kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini.
Uwekezaji huo unaozingatia misingi ya sheria za Kiislamu, ikiwemo kuepuka mifumo ya kifedha inayotumia riba, umetajwa kuwa njia muhimu ya kupanua wigo wa vyanzo vya mitaji na kuongeza ushiriki wa wawekezaji wa ndani na nje katika shughuli za maendeleo.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa fedha Mhandisi Mshamu Ali Munde Katika uzinduzi wa mkutano kwanza wa uwekezaji Kupitia mifumo ya kifedha ya dini ya kiislamu ulioandaliwa na taasisi ya Shirkah asset management Kwa kushirikiana ja CIFCA.
Mhandisi Munde amesema Katika jitihada za kukuza uwekezaji huo, Serikali imeeleza umuhimu wa kukusanya mapato ya ndani pamoja na kuweka mazingira yatakayowezesha kuvutia mitaji kutoka vyanzo mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kwa upande Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirkah ,Salum Awadh amesema mkutano uliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Shirkah na SIFCA umelenga kuangazia maendeleo, fursa, na changamoto za huduma za fedha zinazofuata misingi ya Kiislamu (halali finance) kama vile benki, bima, na uwekezaji.

Amsema Kupitia mkutano huo,umewakutanisha wataalamu mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka mabenki, makampuni ya ushauri na uwekezaji, taasisi za kiserikali (kama CMSA na Benki Kuu, pamoja na wanazuoni na wataalamu wa masuala ya sheria ya Kiislamu kusimamia miongozo.
“Shrikah na SIFCA zimejipa kutoa elimu endelevu kupitia mikutano ya mitaani na kilele cha mkutano mkuu (Summit) kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, huku tukitarajia kuwakaribisha wageni kutoka nchi za jirani katika mikutano ijayo” amesema.

Aidha ameongeza kuwa mchango wa Shirkah unasimama kama kituo maalum cha kukuza utalaamu, kutoa ushauri, na kuwezesha utekelezaji wa mifumo ya fedha ya Kiislamu kupitia ushirikiano na wadau wa ndani na nje ya nchi kama vile taasisi za kimataifa ili kuhakikisha kunakuwa na wataalamu wa kutosha katika sekta hiyo.
Mwisho…
