HAKIKISHENI SHERIA MNAZOZIANDAA ZINAKIDHI MAHITAJI YA SASA NA YA BAADAE” – MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Mwandishi wa A24tv.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, *Mhe. Hamza S. Johari* ameitaka Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kushiriki kikamilifu katika kuandaa Sheria zitakazorahisisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuwa Ofisi hiyo ina nafasi muhimu katika kuhakikisha sheria zinazoandaliwa zinakidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya maendeleo.

 

*Mhe. Johari* ameyasema hayo wakati alipotembelea na kufanya kikao na Menejimenti ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria, Jijini Dodoma tarehe 3 Novemba, 2025.

Habari Picha 22057
Habari Picha 22058
Habari Picha 22056

Akizungumza wakati wa kikao hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unahitaji mifumo imara na ya kisasa ya kisheria inayowezesha kufikiwa kwa malengo ya maendeleo ya Taifa.

 

*“Natarajia Ofisi hii isijikite tu katika kuandaa sheria baada ya kupokea maelekezo, bali ishiriki kikamilifu, kwa kushirikiana na taasisi husika, katika kutambua maeneo yanayohitaji maboresho ya kisheria”.* Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali

 

Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameielekeza Menejimenti ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria, kuandaa mpango wa namna Ofisi itakavyoshiriki katika kuwezesha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kupitia Uandishi, mapitio na uhuishaji wa sheria.

 

*Mhe. Johari* ameipongeza Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kwa utendaji kazi na mafanikio yaliyopatikana katika uandishi wa sheria, mapitio na uhuishaji wa sheria, tafsiri ya sheria na utoaji wa huduma nyingine za kitaalamu.

Habari Picha 22059

 

Awali, akimkaribisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwandishi Mkuu wa Sheria, *Bw. Onorius Njole* ameeleza namna Ofisi hiyo ilivyojipanga katika kuboresha mifumo ya TEHAMA itakayorahisisha Utendaji kazi, ambapo Ofisi hiyo imeanza utengenezaji mfumo wa uandishi wa sheria ujulikanao kama *Legislative Drafiting Management System.*

Habari Picha 22060
Habari Picha 22061
Habari Picha 22062

Vilevile, Mwandishi Mkuu wa Sheria ameeleza kuwa, Ofisi itaendelea kuratibu zoezi la kuwapatia mafunzo Watumishi kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi wao.

Habari Picha 22063

Mwisho….

Share This Article
Leave a Comment