SABAYA AMLILIA HENRY SIKOI, ATOA KAULI NZITO KUHUSU KIFO “KIFO HAKICHAGUI CHAMA.

Geofrey Steven
3 Min Read

Na Geofrey Stephen ARUMERU:

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, amesema kifo hakichagui itikadi za kisiasa, cheo wala hadhi ya mtu katika jamii, akiwataka wananchi kuheshimu marehemu na kuepuka mijadala inayoweza kuongeza maumivu kwa familia zilizofiwa.

Sabaya alitoa kauli hiyo Oktoba 22, 2026, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Olorien, Wilaya ya Arumeru, marehemu Henry Sikoi.

Akizungumza katika shughuli hiyo ya mazishi, Sabaya alisema kifo ni jambo lisiloepukika kwa kila binadamu, bila kujali nafasi yake katika jamii, chama anachokishabikia au cheo alichonacho.

Habari Picha 21884

Alieleza kusikitishwa na tabia ya baadhi ya watu kutumia vifo vya wenzao kuibua mijadala ya kisiasa au kutoa maoni yasiyothibitishwa, badala ya kuwafariji wafiwa na kuheshimu kumbukumbu za marehemu.

“Kifo ni mjumbe katili sana. Kikija kwa wakati wake, lazima kifike. Uwe CCM, Chadema, uwe kiongozi au mtu wa kawaida, kifo hakichagui,” alisema Sabaya.

Habari Picha 21887

Sabaya afichua alivyomfahamu Sikoi
Akizungumzia uhusiano wake na marehemu Sikoi, Sabaya alisema alikutana naye mara moja tu maishani, lakini katika mazungumzo yao alibaini kuwa alikuwa mtu mwenye imani kubwa kwa Mungu na matumaini ya kupona.
Alisema licha ya matumaini hayo, kifo cha Sikoi ni sehemu ya mapenzi ya Mungu, akiwataka wananchi kujifunza kuthamini maisha na kuonesha upendo kwa wenzao wangali hai.

Habari Picha 21885

Sabaya alisisitiza umuhimu wa kuishi kwa upendo, kuheshimiana na kusaidiana, akieleza kuwa hakuna tofauti za kisiasa au kijamii zinazopaswa kuwazuia watu kuungana wakati wa majonzi.

Aeleza kupoteza viongozi wawili ndani ya wiki moja.

Katika salamu zake za rambirambi, Sabaya alisema amepata pigo la kuwapoteza viongozi wawili ndani ya wiki moja, akiwemo mwenyekiti na mjumbe.

Kutokana na hali hiyo, alitoa wito kwa wananchi kuwaombea viongozi wengine ili waendelee kuwa salama na kutekeleza majukumu yao katika jamii.

Habari Picha 21889
Habari Picha 21890
Habari Picha 21891
Habari Picha 21892

Alisema licha ya kushiriki katika shughuli za kisiasa, imani yake kwa Mungu ni sehemu muhimu ya maisha yake, hivyo anaona umuhimu wa kuunganisha ujumbe wa kisiasa na wa kiroho, hasa katika kipindi cha maombolezo.

Sabaya atoa ujumbe wa matumaini kwa wafiwa
Akitoa salamu zake za mwisho kwa marehemu Sikoi, Sabaya alisema anaamini kuwa siku moja watakutana tena katika ufalme wa Mungu, ambako, kwa mujibu wa imani yake, hakutakuwa na tofauti za vyama vya siasa, mauti wala uharibifu.

Alitoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wa Kata ya Olorien kutokana na msiba huo, huku akiwahimiza kuendelea kuwa na imani katika kipindi hicho kigumu.

Habari Picha 21893
Habari Picha 21894
Habari Picha 21895

Sabaya alihitimisha kwa kuwataka wananchi kutanguliza utu, upendo na mshikamano katika maisha yao ya kila siku, akisisitiza kuwa kifo ni ukumbusho wa umuhimu wa kuthaminiana bila kujali tofauti zilizopo kati yao.

MWISHO

Share This Article
Leave a Comment