Viongozi wapya wa Bakwata Kilimanjaro,watakiwa kubuni vyanzo vya mapato

Geofrey Steven
3 Min Read

Moshi,

Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA),mkoa wa Kilimanjaro,limetaka Viongozi wapya walichaguliwa katika baraza hilo,kubuni vyanzo mbali mbali vya mapato na kuacha kutegemea chanzo kimoja ili kujipatia maendelea endelevu

Haya yamesemwa na Sheikh wa mkoa huo Shaabani Mlewa wakati wa uchaguzi wa Viongozi wa baraza hilo kwa nafasi mbali mbali ikiwamo ya Mwenyekiti wa Halmshauri ya Bakwata mkoa pamoja Wajumbe samba mba na Uchaguzi wa Jumuhiya ya Wanawake wa Kiislamu(JUWAKITA),ulifanyika katika ukumbi wa Bakwata mkoani hapa.

Habari Picha 19986
Habari Picha 19985

Akizungumza Augost 16,2026,mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo,amewataka Viongozi hao kuanzi ngazi ya Mkoa ,Wilaya,Kata hadi Msikiti kubuni vyanzo hivyo za mapato ili kuweza kuwaletea Waislamu maendeleo yao na Nchi kwa ujumla

“Ni kweli Viongozi mliopata frsa ya kuwa kiongozi msitegemee ,chanzo kimoja cha mapato ni hatari,kwani kikipata changamoto shughuli za mbali mbali zikiwamo za maendeleo zitakwama nakushindwa kutoa huduma “amesema Mlewa

Mlewa amesema amelazimika kutoa rai hiyo baada ya kuona maeneo mengi mkoani hapo yana frusa nyingi ,ya kuanzishwa vitega uchumi hivyo kuona umuhimu wa kutoa ushauri huo ,kuliko kutegemea chanzo kimoja kikiwamo Sadaka tu ,hapa tubuni vyanzo na kuacha kutegemea msaada kutoka sehemu nyingine.

Habari Picha 19987
Habari Picha 19988

Amesema kubuni vyanzo vya mapato Baraza litakuwa linapata mapato,anataka kusikia sehemu nyingine na kunakuwa na maendeleo ,Wilaya ya Rombo wawe na mkakati wao ,Moshi vijijini na wao wawe na mkakati wao walete uonekane,hii ndiyo tunataka kwa mkoa wa Kilimanjaro washindane katika kuleata maendeleo

Niwapongeze wilaya ya Mwanga ,kazi inaonekana ya ujenzi Ofisi na ujenzi wa Hospital ,Wilaya ya Moshi mjini kwa kazi kubwa mnayoifanya karibu na Uwanja wa Ndege na Wilaya ya Siha kwa kukomboa uwanja na kuanza kuanda mipango ya maendeleo

Kwa upende mwingine ametaka Viongozi hao waliopata nafasi ya uongozi,kila mmoja asimame kwenye nafasi yake ili kuepusha migongano

Wengine ushindwa kusimama kwenye nafasi zao na mwisho wa siku kunakuwa na mgongano isiyo ya lazima,hivyo kila mmoja asimame kwenye nafasi yake ya uongozi aliyopata ili kuleta maendeleo.

Habari Picha 19989
Habari Picha 19990

Ramadhani Molel mmoja ya wajumbe waliopiga kura katika uchaguzi huo, ,amepongeza zoezi hilo la kwani limekwenda vizuri hadi viongozi kupatikana,hivyo kushauri kufanyiwa kazi maelezo yaliyotolewa na Sheikh wa mkoa huu ili maendeleo yaweze kupatikana

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment