BUSANDA YA KUMBUKWA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI LA DKT.SSH.

Geofrey Stephen
1 Min Read

Na Mwandishi wetu

Wananchi wa Jimbo la Busanda, wamepongeza DKT.Jafari Seif kwa kuteuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DKT .Samia Suluhu Hassan Mbunge wao kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia Afya.

Habari Picha 4482

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema ni heshima ya kipekee ambayo haijawahi kutokea tangu jimbo hilo kuanzishwa Ambapo uteuzi huo umeleta faraja na matumaini mapya kwao huku wakieleza kuwa kwa mara ya kwanza Busanda imepata mwakilishi wa ngazi ya Uwaziri serikalini.

Habari Picha 4480

Wameeleza kuwa uteuzi huo unathibitisha dhamira ya Rais DKT.Samia Suluhu Hassan,kuhakikisha maeneo yote yanashirikishwa kikamilifu katika maendeleo ya Taifa hususani kundi la vijana.

 

Sambamba na hilo Wakatoa ombi kwa mbuge wao awajengee barabara ya Geita – Kahama kwa kiwango cha lami kwani kwa kufanya hivyo itafungua fursa za kiuchumi na kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani.

Habari Picha 4481

Pia wakatoa kilio chao kwa Serikali Kwenye Sekta ya afya kupitia Dkt. Jafari ili kuboresha vituo vya afya na zahanati kwa kuongeza dawa, vifaa tiba na huduma za uhakika muda wote ili kupunguza usumbufu kwa wananchi wanaohitaji matibabu.

Habari Picha 4483

 

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment