TSEZA YAVUTIA MIRADI 1,148 YENYE THAMANI YA DOLA BILIONI 15.3.

Geofrey Steven
3 Min Read

Yalenga kuzalisha ajira 344,841; Serikali kuweka huduma za uwekezaji mikoa yote ifikapo 2028

Na Richard Mrusha A24TV

MAMLAKA ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Uchumi Tanzania (TISEZA) imesajili miradi ya uwekezaji 1,148 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 15.32, inayotarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 344,841 katika kipindi cha Julai 2025 hadi Septemba 2026.

Takwimu hizo zinaonesha ongezeko la shughuli za uwekezaji nchini, huku Serikali ikiendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kupitia kurahisisha taratibu za usajili, vibali na upatikanaji wa huduma mbalimbali.

Habari Picha 22050

Hayo yamebainishwa Leo Novemba 2,2026 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mkuu wa TISEZA,
Gilead Teri amesema mtaji huo,wa uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ya nchi (FDI) umechangia Dola bilioni 9.6, wakati wawekezaji wa ndani wakichangia Dola bilioni 5.72.

Hatua hiyo inaonesha nafasi ya mtaji wa ndani katika kukuza uchumi wa taifa, sambamba na umuhimu wa kuvutia mitaji kutoka nje kwa ajili ya kuongeza uzalishaji, kuhamisha teknolojia na kupanua wigo wa ajira.

Aidha,amesema TISEZA iliundwa Julai Mosi, 2025 kupitia Sheria Na. 5 kwa kuunganisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), kwa lengo la kuimarisha uratibu wa uwekezaji na kutoa huduma katika mfumo mmoja.

Amesema kuwa Kupitia mfumo huo wa Kituo cha Pamoja cha Huduma kwa Wawekezaji (One-Stop Centre), mamlaka hiyo inaratibu huduma za takribani taasisi 16 za Serikali, zikiwemo BRELA, TRA, Idara ya Ardhi, TMDA, OSHA, Uhamiaji, Wizara ya Kazi na Tume ya Madini.

Amesema Mfumo huo unalenga kupunguza urasimu na muda unaotumika na wawekezaji kutafuta vibali na huduma kutoka taasisi mbalimbali, hivyo kuwawezesha kuanza shughuli zao kwa urahisi zaidi.

Habari Picha 22049

Ameongeza kuwa Katika kuongeza fursa za uwekezaji, Serikali pia imeendelea kuendeleza maeneo maalum ya uchumi (Special Economic Zones), ambayo yameandaliwa kwa miundombinu na taratibu zinazolenga kurahisisha uanzishaji wa viwanda na shughuli za uzalishaji.

Maeneo matano yaliyopewa kipaumbele ni Bagamoyo Maritime City, Kwala mkoani Pwani, Nala mkoani Dodoma, Mbinga/Songea na Buzwagi iliyopo Kahama, huku maeneo mengine zaidi ya 20 yakitajwa kuwepo nchini.

Aidha, TISEZA imeweka mkakati wa kupanua huduma zake katika mikoa yote nchini ifikapo mwaka 2028, ili wawekezaji waweze kupata huduma karibu na maeneo wanayokusudia kuwekeza bila kulazimika kutegemea ofisi za makao makuu pekee.

Habari Picha 22051

Kwa sasa huduma hizo zinapatikana katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Mbeya, Iringa, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Kigoma, Mtwara na Tanga.

Amesema taarifa hizo zinaeleza kuwa ofisi za mamlaka hiyo hupokea kati ya wageni na wawekezaji 200 hadi 250 kwa siku, hali inayoonesha mwitikio wa wawekezaji wanaotafuta fursa na taarifa za uwekezajih nchini.

Amesema kuwaKwa ujumla, mafanikio ya kuvutia uwekezaji hayapimwi kwa idadi ya miradi iliyosajiliwa pekee, bali pia uwezo wa kuifanya miradi hiyo kuanza uzalishaji, kutoa ajira zilizokusudiwa, kuongeza mapato ya Serikali na kuchochea ukuaji wa viwanda na uchumi wa wananchi.

Habari Picha 22052

Mwisho…

Share This Article
Leave a Comment