Na Mwandishi wa A24tv.
AUMS imefungua Kituo cha Mafunzo (Training Center) mkoani Geita, kinacholenga kuwajengea uwezo vijana na watoto wa Kitanzania kuendesha mitambo na mashine kubwa za migodini, hususan katika uchimbaji wa chini ya ardhi (Underground Mining).
Kampuni ya African Underground Mining Services (AUMS) imeeleza jinsi inavyoendelea kuchangia maendeleo ya jamii mkoani Geita, huku ikijivunia kuwa miongoni mwa wakandarasi wakuu wa uchimbaji wa chini ya ardhi nchini.
Akizungumza Leo Septemba 26,1026 kwenye Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, mkoani Geita Mratibu wa Maudhui ya Ndani wa kampuni hiyo, Saad, Simba amesema kampuni yao imejikita katika kuhakikisha Watanzania wananufaika moja kwa moja na sekta ya madini.

Amesema kwa sasa asilimia 98 ya manunuzi yote ya kampuni yanafanyika ndani ya Tanzania, hatua inayolenga kuziwezesha kampuni za ndani na kuchochea mzunguko wa fedha nchini.
“Tunatoa fursa za ajira kwa Watanzania na kuziwezesha kampuni za ndani kukua. Huu ndio maana halisi wa Local Content,” amesema Saad.
Saad ameeleza kuwa kampuni hiyo inashirikiana kwa karibu na Tume ya Madini pamoja na Wizara ya Madini katika kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya sekta hiyo.
Kwa upande wa miradi, alisema nchini Tanzania kwa sasa wana mradi mkuu wa AngloGold Ashanti (Geita Gold Mine) ambao ndio mradi wao pekee wa underground, huku kimataifa kampuni mama ikiendelea kufanya kazi katika nchi kama Misri, Ghana, Australia na Amerika ya Kaskazini.
Maonesho hayo yenye kaulimbiu isemayo _Kuwezesha Wachimbaji Wadogo Kuongeza Tija Kujenga Sekta Imara yamekuwa jukwaa muhimu kwa kampuni za ndani na za kimataifa kuonesha mchango wao katika ukuaji wa uchumi wa madini nchini.
Mwisho
