TAWA YAONGEZA MAZAO YA VIVUTIO SABASABA.

Geofrey Steven
1 Min Read

Na Richard Mrusha

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imesema ushiriki wake katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam Sabasaba unalenga kutoa elimu ya uhifadhi wa wanyamapori, kuhamasisha utalii wa ndani, pamoja na kusogeza huduma kwa wananchi kupitia maonesho ya wanyamapori na uuzaji wa nyara halali za wanyamapori na nyama pori.

Habari Picha 19107

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Julai 3, 2026, Mhifadhi Mkuu wa TAWA, Steven Madenge, amesema wananchi wanaotembelea banda la mamlaka hiyo wanapata fursa ya kujionea wanyamapori mbalimbali wakiwemo twiga, simba, chui, fisi, pundamilia, tembo na mamba, hatua inayolenga kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa uhifadhi na kuwavutia kutembelea hifadhi za wanyamapori nchini.

Habari Picha 19106

Aidha, amewataarifu wananchi kuwa TAWA imeandaa programu mpya iitwayo Pande Marathon, inayotarajiwa kufanyika Agosti 1, 2026 katika Hifadhi ya Pande, jijini Dar es Salaam, amesema mbio hizo zinalenga kuimarisha afya pamoja na kuendelea kuunganisha wananchi na shughuli za utalii na uhifadhi nchini.

Habari Picha 19108

Mwisho.

Share This Article
Leave a Comment