CCM NA CHADEMA WAZIBE PENGO LA CARDINAL PENGO KWA MKONO WA HERI NA TABASAMU

Geofrey Stephen
2 Min Read

*CCM na CHADEMA wazibe pengo la Cardinal Pengo kwa kunyosheana mkono wa heri na uso wa tabasamu.(maridhiano)*

Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa mang’amuzi yake kwa viongozi wa CCM na CHADEMA kwa kutambua zawadi ya maisha ya marehemu Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo (Kuhani) kupitia salaam za Rambirambi.

 

Habari Picha 7250

Kwenye salaam za Rambirambi vyama hivi viwili vikubwa nchini vimemwelezea marehemu kuwa alikuwa mtu mnyenyekevu,mpenda mshikamano wa kijamii,mtu aliyeishi maadili ya haki,amani upendo.

Mimi kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kusukuma Maridhiano ya Kitaifa (KKMK) nimevutiwa na kujawa na furaha na matumaini kwa kusoma maneno mazuri yenye Uungu ndani mwake kuhusu zawadi ya maisha ya marehemu Polycarp Cardinal Pengo.

Wito wangu kwa CCM na CHADEMA

Kama ambavyo wametambua tunu ya *unyenyekevu* , *haki,amani,mshikamano* ambayo Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo aliishi basi ni matumaini kwamba viongozi hawa watamwaibisha shetani hadharani na kuelekea na kisha kukumbatia kwa ujasiri Unyenyekevu, Haki,Mshikamano, Amani na Upendo wakati huu ambapo Taifa linahitaji kuponywa na kujengwa upya.

Ni matumaini na faraja kwamba tarehe 28 siku ambayo mwili wa Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo utarudishwa kwenye makazi ya milele na roho yake ikipaa kwenda kufurahi na kuburudika kwa Baba (Muumba) viongozi wetu Rais Samia Suluhu Hasaan kwa niyaba ya Serikali,John HECHE kwa niyaba ya CHADEMA Mzee Wassira kwa niyaba ya CCM wataonesha kwa vitendo tunu alizoishi Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo kwa kupeana mkono wa heri,busu lililo takatifu ,uso wa tabasamu wenye kuashiria mwanzo mwema wa Taifa na bila shaka Rais aweza kutumia jukwaa hilo kutangaza uhuru kwa wanasiasa wenzake walioko gerezani akiwemo TUNDU LISSU.

Tusherehekee maisha ya Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo ambaye alikuwa chombo cha Majadiliano na maridhiano.

Bila shaka faraja na raha ya milele ya Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo itakamilika pale atakapoona roho ya mazungumzo na maridhiano yanatamalaki nchini.

Mbele Kuna Mwanga

Odero Charles Odero

Mwenyekiti wa Kamati ya Kusukuma Maridhiano ya Kitaifa (KKMK)

20.02.2026

Share This Article
Leave a Comment